Habari za Punde

TAMWA yaandaa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari

Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa Ally akieleza umhimu wa wanahabari katika kuwainua wanawake kwenye jamii ikiwemo kushika nafasi za uongozi.


Mwandishi wa habari Mwandamizi wa gazeti la Habari leo Khatib Sleima(Gurecha )alipkua akitoa neno la kuhamasisha waandishi wa habari vijana kufanya kazi za kuwaibua wanawake.
Baadhi ya wanahabari wakiendelea kufanyia kazi za makundi kabla ya kuwasilisha kazi hizo.
Mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt,Salum Sleiman akiendelea na mafunzo kwa waandishi wa habari Zanzibar.

Mjumbe wa Chama cha Waandishi wa habari TAMWA-Zanzibar Bi Ummy Alley akitoa nasaha zake wakati alipokua akifungua mafunzo ya siku mbili kwa baadhi ya waandishi wa Habari Zanzibar yanayohusu umuhimu wa kuwaunga mkono wanawake na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wanahabari,mafunzo haya yamefanyika katika ofisi za TAMWA,Tunguu.


Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa-Zanzibar DKt,Mzuri Issa Ally amesema waandishi wa habari ni watu muhimu na wenye mchango mkubwa wa kuwasaidia wanawake wa Zanzibar kufikia malengo yao ikiwemo ya kushika nafasi za uongozi.

 

Aliyasema hayo katika ofisi za Chama hicho zilizopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari 40 kutoka vyombo mbali mbali.


Mafunzo hayo ya siku mbili yalilenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutambua umuhimu na mchango wa mwanamke kwenye jamii sambamba na matumizi sahihi ya mitandao mkwa waandishi wa habari.

 

 

Alisema wakati wanahabari wanatekeleza majukumu yao ya kila hawana budi kukumbuka na kuweka mbele umuhimu wa wanakawake katika habari zao za kila siku kwa kuwa baadhi ya waandishi wa habari husahau wajibu huo.

 

‘’Nyinyi ni sauti ya wasio na sauti jifunze mafunzo haya kisha nendeni mkayafanyie kazi kwa kuinua jamii ya wanawake.

 

Awali akifungua mafunzo hayo mjumbe wa TAMWA Bi Ummy Alley aliwataka wanahabari vijana kujifunza kwa waliowatangulia ili waweze kuwa bora zaidi.

 

Alisema taaluma ya habari ni muhimu mmno ambayo inachangaia kuleta mabadiliko na uwajibikaji katika taasisi mbali mbali iwapo itafanywa vyema.

 

Awali Mwandishi wa habari mkongwe Zanzibar kutoka gazeti la habari leo Khatib Sleiman aliishukuru TAMWA kuendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari hususani vijana.

 

Sambamba na hayo Khatibi alizungumzia kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa usahihi mkubwa ikiwemo kuwafikia vyanzo vyao vya habari popote pale walipo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.