Kampuni ya kimataifa ya Millicom International Cellular S.A ambayo ni kampuni mama ya kampuni za Tigo na Zantel inatangaza kuwa imeingia katika makubaliano na Axian Group, kampuni ya kimataifa iliyoko Antananarivo - Madagascar ili kuiuzia umiliki wa kampuni hizo mbili zilizopo Tanzania.
Hatua ya kuziuza kampuni hizo kwa Axian
Group ni sehemu ya mkakati wa Millicom kujikita katika utoaji wa huduma za simu katika ukanda wa America ya Kusini (Latin America) baada ya kufanya uwekezaji mkubwa katika kuendeleza sekta ya mawasiliano barani Afrika kwa takribani miaka
25.
Ujio wa kampuni ya Axian Group
kwenye soko la Tanzania
utawezesha kuongeza wataalamu katika sekta ya mawasiliano ambao wamefanikiwa kutengeneza na kukuza nembo na biashara nyingi katika ukanda wa bahari ya
Hindi, Afrika pamoja na Ulaya.
Axian Telecom
ni moja ya kampuni tanzu inayoongoza kutoa huduma za mawasiliano nchini Madagascar,
Visiwa vya Reunion, Mayotte na Comoro pamoja na nchi za Senegal na Togo.
Millicom inafarijika kumpata muwekezaji mahiri kama Axian ambaye amejizatiti katika kuendeleza mipango ya muda mrefu iliyowekwa na Tigo na
Zantel ili kuhakikisha zinatoa huduma nafuu, za uhakika na za kibunifu kwa watanzania.
Katika kutekeleza hayo,
Axian imepanga kufanya yafuatayo:
· Kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ili kuongeza ushindani,
kuboresha uendeshaji pamoja na kuhakikisha mageuzi ya uchumi wa kidigitali.
· Kupanua wigo wa huduma za mawasiliano na kuchochea mageuzi ya kidigitali katika nchi ya
Tanzania.
· Kuchochea ujumuishwaji wa watu kiuchumi ‘Financial Inclusion’ pamoja na kuongeza ubunifu kwenye huduma za fedha·
Kuhimiza ukuaji wa taaluma kwa wafanyakazi kupitia mafunzo ili kufanikisha malengo yaliyowekwa Tuna penda kuwahakikishia wadau na umma kwa ujumla kuwa, uendeshaji wa biashara utabaki kama ulivyo hadi pale tutakapopata vibali na uthibitisho kutoka kwa mamlaka husika. Pia tutaendelea kuwapa wateja wetu bidhaa na huduma bora.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka
1995, Kampuni ya Millicom Tanzania (Tigo) kupitia azma yake ya kuleta mageuzi ya kidigitali,
ilikuwa ya kwanza kuzindua GSM na mtandao wa 3G nchini Tanzania.
Mnamo Aprili
2014, Tigo ilizindua mtandao wa 4G katika jiji la Dar es Salaam na ilipofika mwaka
2016, mtandao wa 4G ulikuwa umeenea katika mikoa yote ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment