Habari za Punde

 

JAMHURI ya Muungano wa  Tanzania, ikiwemo Zanzibar,  imekuwa ikifanyakazi na mataifa mbali mbali duniani katika kudumisha amani pamoja na kutafuta suluhu ya migogoro kadhaa na kuimarisha usalama na maendeleo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema katika hotuba yake wakati alipoungana na viongozi kadhaa duniani kwa njia ya mtandao katika kujadili njia bora za kuimarisha umoja na mshikamano ambapo mada kuu ilikuwa ni “Kuimarisha umoja kwa kuleta na kudumisha amani hasa katika Rasi ya Korea (Korea Peninsula).

Mjadala huo ambao umefanyika kwa njia ya mtandao kutokana na uwepo wa maradhi ya COVID 19 duniani, Rais Dk. Mwinyi alianza kwa kumpongeza Dk. Hak Jan Han mwanzilishi wa Taasisi ya “Universal Peace Federeratio” kwa kumpa fursa hiyo ya kuungana na viongozi kadhaa duniani katika mjadala huo.

Katika mjadala huo ambapo miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa ni kuwataka viongozi wa dunia siyo tu kuzungumzia matatizo ya kuzuka kwa maradhiya COVID 19, bali pia,kuwanafikra mpya za kuondokana na matatizo yaliyopo na badala yake kuwa wamoja katika hali ya usalama na amani duniani.

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa ingawa kijiografia Rasi ya Korea inaonekana iko mbali na Afrika, lakini ikumbukwe kwamba licha ya umbali huo, Afrika imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kurejesha hali ya amani na demokrasia katika eneo hilo.

Alisema kuwa kwa bahati mbaya, licha ya juhudi zilizochukuliwa na Jumuiya za Kimataifa, hadi leo eneo hilo bado limebaki na mivutano ambayo inatishia usalama katika eneo la Kusini Mashariki ya Bara la Asia na kutoa changamoto kadhaa kwa usalama wa dunia kwa jumla.

“Hatuwezi kuendelea kubaki tunautizama tu mgogoro huo, ambapo baadhi ya wakati unajulikana kuwa ni ‘mgogoro uliosahauliwa ambapo kuwepo kwa mgogoro huu kuna athari nyingi kwa amani na usalama wa dunia”,alisema Dk. Mwinyi.

Kwa msingi huo, Rais Dk. Mwinyi alitoa pongezi kwa Dk. Han Ja Han, kwa kukusanya timu ya wataalamu kutoka pande mbalimbali za dunia ili waje na rai na fikra mpya zenye lengo la kurejesha hali ya amani na usalama ili kuwa na Korea  iliyoungana.

Akizungumzia hali ya Kisiasa ya  Zanzibar  na historia yake, Rais Dk. Mwinyi alimpongeza Marehemu Seif Sharif Hamad, kwa kukubali kuungana naye katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo matokeo ya Uchaguzi mkuu yalimueezesha kumteua kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Alieleza alivyofarajika kwa uamuzi huo wa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambapo ni miongoni mwa mafanikio makubwa aliyoyapata ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano atakachokuwepo madarakani.

Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa lengo lake ni kuona kuwa kuna Zanzibar ambayo watu wake  ni wamoja na inapiga hatua za haraka za maendeleo.

 Alisema jinsi anavyoamini kuwa hali ya amani na utulivu ndiyo chachu ya maendeleo ya Zanzibar na anahisi hivi sasa Zanzibar imepiga hatua katika kusaha utofauti zilizokuwepo na kuondoa changamoto zilizokuwa zinakwaza maendeleo.

 Alisisitiza kwamba Zanzibar imedhamiria kutumia vizuri rasilimali zake na fursa iliyopo kijiografia ya kwamba Zanzibar iko eneo zuri,  eneo la kimikakati na muhimu katika kuendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi.

Alifahamisha kuwa Serikali anayoiongoza imejidhatiti kuimarisha na kukuza fursa za uwekezaji na kutoa upendeleo maalumu kwa wawekezaji wanaowekeza Kisiwa cha Pemba ili kukuza maendeleo katika kisiwa hicho na kuleta uwiano wa kasi na hali ya maendeleo baina ya Kisiwa cha Unguja na Kisiwa cha Pemba.

“Kuhusu dhamira na malengo yangu niliyonayopanga kuyatekeleza kwa Zanzibar baada ya uchaguzi kwa ufupi, naweza kusema kwamba ni kuendeleza uchumi wa buluu kwa kushirikiana kwa karibu sana na sekta binafsi ili kuweza kufikia malengo yangu ya kuifanya Zanzibar kuwa ni kitovu cha biashara katika ukanda wa Bahari ya Hindi”,alisema Dk. Mwinyi.

 Aidha, alisemakuwa Zanzibar inafursanarasilimalinyingizakuwezakuendelezauchumiimarautakaowezakukuzaajira, kupunguzaumasikininahatimaekupatamaendeleoyaharaka.

 

AliongezakuwaZanzibar imedhamiriakuendelezauchumiwabuluukwakushirikianananchiwanachamawaJumuiyayaNchiZinazopakananaBahariya Hindi (IORA)  ambazonazokwaupandewaozimepangakuendelezauchumihuo.

 

AlisisitizakwambaJamhuriyaMuunganowa Tanzania, ikiwemo Zanzibar itafaidikasanakwakuimarishaushirikianonanchihizokatikakuendelezauchumiwabuluu.

 

Rais Dk. MwinyialielezakwambaSerikalianayoiongozaitahakikishakwambakatikautekelezajiwamipangoyamaendeleoinashirikiananaWashirikawamaendeleoilikuwezakufikiamalengoyakeyakukuzaajira, kuimarishasektayaelimu, afya, namiundombinukwakuzingatiaDirayaMaendeleoya Zanzibar yaMwaka 2050.

 

Rais Dk. Mwinyialimuungamkono Dk. Hak Jan Han, pamojanawanachamanamarafikiwotewataasisiya“Universal Peace Federation”naJumuiyazakekatikakuimarishaamaninakuharakishamaendeleo.

 

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.