Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Suleiman Hemed Abdulla Amekutana na Wasimamizi wa Mfumo wa SNR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akipata maelezo ya Mfumo wa Sema na Rais Mwinyi (SNR) kutoka kwa Mtaalam anayesimamia mfumo huo Ndg. Haji Khamis Makame, wakati wa mazungumzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Ofini ya Makamu Vuga Jijini Zanzibar. 

Na.Kassim Abdi.OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla anatarajia kukutana na wasimamizi wa mfumo wa sema na Rais (SNR) mfumo ambao unatarajiwa kuwa chachu ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Mhe. Hemed amefikia uwamuzi huo mara baada ya kufanya mazungumzo na wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Bwa. Mohamed Hashim Rakii na Haji Khamis Makame wanasimamia mfumo huo Afisini kwake Vuga jijini Zanzibar.

Wataalamu hao wamemueleza Makamu wa Pili wa Rais kuwa zimekuwepo baadhi ya changamoto zinazowakabili wasimamizi wa mfumo wa sema na Rais mwinyi ikiwemo kukosa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya wakuu wao wa taasisi.

Wamesema tangu kuzinduliwa kwa mfumo huo wananchi pamoja na watendaji wengi wamejitokeza kutuma kero na changamoto zinazowakabili lakini kumekuwa na tatizo la uchelewashaji wa kupatina majibu kwa muda unaostahili.

Walimueleza Makamu wa Pili wa Rais kwamba mfumo wa sema na Rais Mwinyi ni kiunganishi Muhimu katika kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi endapo utasimamiwa na kufanyiwa kazi kwa umakini.

Akijibu changamoto zilizowasilishwa na wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Mhe. Hemed amesema ili kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo anakusudia kuktana na wasimamizi wa mfumo huo kwa lengo la kuskiliza changamoto wanazokabiliana nazo na kuzipatia ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Amesema wananchi wamekuwa na matumaini makubwa na serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais Dk. Mwinyi hivyo kuna kila sababu kwa watendaji wanaosiamamia taasisi za serikali kufanya kazi kwa uweledi ili kufikia lile lengo la wananchi kwa serikali yao.

Makamu wa Pili wa Rais ameleza kuwa anakusudia kuonana na Wasimamizi wa mfumo huo siku ya Jumatano ya terehe 26 Mei, 2021 ili kuskiliza changamoto zao na  siku hio hio atazungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa maelekezo kwa wakuu na wasimami wa Taasisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.