Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Bara, Philip Mangula, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan  akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 07 Mei, 2021katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam

 

Sehemu ya Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kwa ajili ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam

Viongozi wa Kidini, Viongozi Wakuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiomba Dua kabla ya kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipohutubia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.