Habari za Punde

Habari za hivi Punde: Ajali mbaya ya Basi yatokea Shinyanga, wanafunzi watatu wafariki dunia


Watu watatu wamefariki dunia na wengine 31 kujeruhiwa baada ya Basi la Classic lilitoka Kampala, Uganda kuelekea Dar eneo la Buyubi Shinyanga. 


Waliofariki 3 kati yao wanafunzi wawili na mlezi mmoja wa mototo wa mwanafunzi (care taker "yaya")

Majeruhi wa kawaida 31


Wenye hali mbaya ni wawili ambao kati yao wapo waliopoteza viungo vya mwili.

Kwa sasa wanakusanywa eneo moja kwani waliwekwa Hospitali mbili tofauti.

Marehemu ni:

1) Wahda Yusuph (Bsc Nursing)
2) Nassor Juma Khamis (Bsc Nursing)
3) Rehema Haji Juma (care taker)

Kwa mujibu wa orodha inaonekana hawa wanatokea Zanzibar.

Wizara ya Mawasiliano TSAU Tunaendelea kupata taarifa za majeruhi na mahututi.

Mungu azilaze roho za marehemu wote mahala pema peponi na Majeruhi wote wapone haraka.

Idara Ya Mawasiliano
TSAU


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.