Habari za Punde

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Akutana na Uongozi wa Bodi ya NEMC.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary  Maganga akiongoza Kikao cha Viongozi wa Bodi na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) leo Juni 25, 2021 jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Bi. Mary aliwataka Viongozi hao kutimiza wajibu wao katika kusimamia Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 ikiwemo masuala ya vibali vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA), Taka Hatarishi na Usimamizi wa Fedha.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.