Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akijumuika na Viongozi na Waislamu kumswalia Marehemu Mzee Msuri Muhidini aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mjini pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mikunguni Jimbo la Kwahani, Swala iliongozwa na Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Hassan Othman Ngwali (mbele) katika Msikiti wa Muembe Mimba Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo,Marehemu atazikwa Kijijini kwao Unguja Ukuu Kaebona Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akijumuika na Viongozi na Waislamu kuitikia dua iliyoombwa baada ya kumswalia Marehemu Mzee Msuri Muhidini aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mjini pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mikunguni Jimbo la Kwahani, katika Msikiti wa Muembemimba Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo,Marehemu atazikwa Kijijini kwao Unguja Ukuu Kaebona Wilaya ya Kati Unguja.
Alhaj Dk. Mwinyi aliwaomba wana familia kuwa na subira katika kipindi hichi kigumu cha msiba wa mzee wao Marehemu Mzee Msuri Muhidini ambaye ameacha kizuka mmoja na watoto wanne na kumuombea kwa MwenyeziMungu ailaze roho yake marehemu mahala pema peponi, Amin.
Hadi anafariki dunia Marehemu Mzee Msuri Muhidini alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mjini ambaye pia, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Tawi la Mikunguni, Jimbo la Kwahani katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
No comments:
Post a Comment