Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan atembelea na kukagua Daraja la JP Magufuli lenye Urefu wa Km 3.2 (Kigongo -Busisi) mkoani Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Eng. Patrick Mfugale ambaye alikuwa akielezea hatua za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 linalounganisha kati ya Wilaya ya Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza ambapo limefikia asilimia 27, huku Daraja la kupitisha vifaa likiwa limekamilika kujengwa kwa asilimia 100.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) Eng. Patrick Mfugale ambaye alikuwa akielezea jinsi ya kushusha nondo zilizosukwa katika umbo la duara katika mashimo marefu yaliyochimbwa ndani ya maji ya ziwa Victoria (haonekani pichani)
Nondo zilizosukwa kwa umbo la duarazikishushwa ndani ya moja ya shimo refu lililochimbwa ndani ya maji ya ziwa Victoria katika hatua zinazoendelea za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 Kigongo mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ujenzi wa moja na Nguzo ambayo imeshawekewa zege katika muendelezo wa kazi za ujenzi wa Daraja la JP Magufuli lenye urefu wa Kilometa 3.2 Kigongo mkoani Mwanza.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.