Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Amepokea Ujumbe Maalum Kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe.Paul Kagame, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kumkaribisha Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta mara baada ya kuwasili Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 03 Juni, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta mara baada ya kuwasili Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisoma Ujumbe huo Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kuwasilishwa kwake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta wapili kutoka (kushoto) wakwanza (kulia) ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na wakwanza kushoto ni Balozi wa Rwanda hapa nchini Meja Jenerali Charles Karamba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na mgeni wake Mjumbe Maalumu wa Rais wa Rwanda Paul Kagame, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda Dkt. Vincent Biruta mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 03 Juni, 2021.PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.