Na John Mapepele, Mtwara
Naibu waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul (Mb) ameitaka Kamati
ya Kitaifa ya UMITASHUMTA na MISSETA kutoa muongozo wa kuhahikisha watoto wa Shule
za Serikali na watu binafsi wanashiriki kikamilifu katika mashindano haya ili
kujenga umoja, uzalendo na mshikamano kwa watoto wa Tanzania.
Mhe.
Gekul ametoa kauli hiyo leo Juni 18, 2021 wakati akifunga mashindano ya UMITASHUMTA
kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ambapo amesisitiza kuwa Malengo
ya mashindano haya ni kutoa fursa kwa wanafunzi wa Shule za Msingi kushiriki na
kuonesha vipaji vyao vya michezo na sanaa walivyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Amesema kwa mara ya kwanza katika
historia ya michezo hii, mashindano ya 25 ya mwaka 2021 yameratibiwa kwa pamoja
na Wizara tatu ambazo ni; Ofisi ya Rais TAMISEMI; Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo pamoja na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambapo amesisitiza kwamba
uratibu huu umesaidia kufanikisha maandalizi na uendeshaji wa michezo hii kwa
ufanisi mkubwa.
Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa maelekezo
aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri Mkuu wakati alipokuwa akifungua mashindano hayo
Juni 8, mwaka huu kuhusu kuimarisha ufundishaji wa somo la michezo
na michezo katika ngazi zote za elimu Mhe. Gekul amesema.
“Katika
kutekeleza hili tunakusudia kufanya yafuatayo; kufanya tathimini ya mitaala ili
kubaini mapungufu na kuiboresha, kuhuisha vyuo vya ualimu vya michezo na
kuboresha ufundishaji wa elimu kwa michezo kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya
ualimu ili wahitimu wake wote wawe na stadi ya ufundishaji wa somo la elimu kwa
michezo”.
Ameongeza
kuwa tayari, Wizara hizi tatu zipo katika maandalizi ya awali ya kuanzisha tahasusi
za elimu kwa michezo kwa kidato cha 5 na 6.
“Hata hivyo imebainika kuwa katika mashindano
haya baadhi ya mikoa imewaleta wachezaji ambao hawana sifa ya kushiriki
mashindano ya UMITASHUMTA (Mamluki). Jambo hili nalikemea kwa nguvu zote na
naelekeza mamlaka za kinidhamu kwa wote waliohusika na jambo hili kuchukua hatua
stahiki mara moja. Ili kuhakikisha kwamba suala kama hili
halijitokezi tena katika mashindano haya naielekeza Kamati ya mashindano
kuhakikisha kuwa muungozo wa uendeshaji mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA unaoandaliwa
unaweka utaratibu na kanuni zitakazodhibiti kabisa suala hili” amefoka Mhe.
Gekul
Katika
mashindano hayo alitoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa jumla ambapo mkoa wa
Mara uliibuka mshindi wa jumla wakati Mkoa wa Dar es Salaam uliibuka bingwa kwenye
fainali za mchezo wa soka kwa wavulana uliochezwa na timu ya Mkoa wa Mara kwa kuichapa
Mara magoli manne kwa sifuri mbele
ya mgeni rasmi Mhe. Gekul
Mratibu
wa mashindano hayo Leonard Thadeo amesema
mashindano yam waka huu yamekuwa na hamasa kubwa na kwamba kila mkoa umejitahidi kuonesha kiwango cha hali ya juu tofauti na miaka iliyopita.
Amesema
tayari kamatiimeshawachagua wanaliadha kumi waliofanya vizuri ili waweze kushisiki
kwenye mashindano ya Dunia ya Riadha kwa wanafunzi kati
ya miaka 13-15 yatakayofanyika
nchini Serbia mapema Septemba mwaka huu.
Amezizitiza
kuwa lengo kubwa la mchezo hii siyo kuangalia ushindi wa kupata kombe bali
kuangalia jinsi ya kuwafanya watoto wapate furaha na kujenga misingi ya upendo
na uzalendo kwa kizazi cha sasa.
No comments:
Post a Comment