Habari za Punde

Wananchi Wahimizwa Kuwa na Mashirikiano ya Pamoja Kupiga Vita Dhidi ya Uingizaji na Utumiaji wa Dawa za Kulevya

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungmza na waumini wa Masjid Nouri Kombeni Wilaya ya Magharibi "B"Ungyuja  mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa akiwahimiza kuwa na mashirikiano ya pamoja katika kupiga vita dhidi ya Uwingizaji, Usambaji na Utumiaji wa Dawa za Kulevya.
Waumini waliotekeleza ibada ya Sala ya Ijumaa katika Masjid Nouri Kombeni Wilaya ya Magharibi "B" Ungyuja wakimskiliza kwa makini wakimsiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla wakati akitoa salamu zake alipokaribishwa na Uongozi wa Mskiti huo kuzungumza na Wananchi baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa.




Na.Kassim Abdi.OMPR Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kupiga vita dhidi ya uwingizaji, usambazaji na utumiaji madawa ya kulevya Nchini.

Mhe. Hemed alitoa wito wakati akitoa salamu zake kwa waumini wa Masjid Nouri Kombeni Mkoa wa Mjini Magharibi mara baada ya kukamika kwa ibada ya sala ya Ijumaa.

Alisema umefika wakati wananchi wa Zanzibar kuungana pamoja katika kupiga vita Madawa ya kulevya  ili kuikoa jamii na athari zitokanazo na madawa ya kulevya.

Mhe. Hemed alieleza kuwa iwapo jamii itachukuwa jitihada za maksudi za kuwafichua wahusika wa mtandao wa dawa za kulevya Zanzibar itakuwa salama kutokana na wasambazaji na watumiaji kuwemo ndani ya jamii.

“ Ni wajibu kila mmoja kuondoa hofu katika  kutoa taarifa kwani serikali imejipanga vyema katika kuondoa kabisa suala kadhia hii inayoangamiza vijana wetu na jamii kwa ujumla”  Alieleza Mhe. Hemed

Akigusia suala la sheria juu ya madawa ya kulevya Makamu wa Pili wa Rais  alisema serikali haitasita kuifanyia marekebisho sheria hiyo kama ilivyochukua hatua katika sheria nyengine ili kwa lengo la kuwabana wahalifu wa vitendo hivyo.

Akizungumzia juu ya maradhi ya Covid - 19 alitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari juu ya wimbi la tatu linalotarajiwa kuikumba dunia kwa kutumia njia ya kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka, kuepuka kikusanyiko pamoja kuvaa barakoa.

Mapemma khatibu wa mskiti huo Shekh Abdallah Juma Mussa aliwataka waumini wa dini ya kiislamu kuijenga jamii katika maadili mazuri  ili kupunguza vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za kuelvya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.