Habari za Punde

WATANZANIA MSIMUACHE MUNGU KATIKA MAPAMBANO YA CORONA: RAIS SAMIA

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC katika ukumbi wa AMECEA Kurasini mkoani Dar es Salaam leo 25 Juni, 2021.

Na. Georgina Misama                                                                                  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kila mmoja kwa dini yake wasiache kumuomba Mungu katika kupambana na ugonjwa wa corona sambamba na tahadhari mbalimbali ambazo zinachukuliwa katika kuepusha maambukizi ya ugonjwa huo.

Akihutubia leo Jijini Dar es salaam katika mkutano maalum na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC),uliofanyika katika ukumbi wa Kurasini Jijini Dar es Salaam, Rais Mhe.Samia alisema kwamba Dunia hivi sasa inakabiliwa na ugonjwa wa Covid 19 wimbi la tatu na Tanzania ina wagonjwa waliopata maambukizi hayo hivyo basi amewaomba Maaskofu pamoja na viongozi wa dini mbalimbali kumlilia Mungu kwani yeye ni muweza wa yote.

“Nawaomba Maaskofu pamoja na viongozi wengine wote wa dini nchini pamoja na njia zote za kisayansi tutakazo zitumia tusisahau kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutuepesha na kutuhifadhi na maradhi haya kwani yeye ndie muweza wa yote. Nimeangalia kwenye kitabu nilichonacho na nimeona kwenye Zaburi 91:4 kuna maneno ya Daudi napenda kumnukuu, ‘Mungu atakufunika na mbawa zake na chini ya mbawa zake utapata hifhadhi, uaminifu wake kwa waja wake utakuwa ndio ngao na ngome yetu utapata usalama kwake’ na ndiyo maana na sisitiza tumuombe Mungu, atuwekee mkono, atufunike na mbawa zake”, alisema Rais Mhe.Samia

Aidha, Rais Samia alifafanua kwamba Dunia hivi sasa inapita katika wimbi la tatu la ugonjwa wa Corona ambapo Tanzania ilipitia kwenye wimbi la kwanza na la pili na sasa hivi inakabiliwa na wimbi la tatu kwani ishara za kuwepo kwa wagonjwa waliopata maambukizi hayo ndani ya nchi zinaonekana.

Pamoja na hayo, Rais Samia ametambua msimamo dhabiti wa Kanisa Katoliki katika kupambana na ugonjwa huo na kuwataka viongozi wa dini nchini kuwakumbusha waumini wao, umuhimu wa kujikinga na kuchukua tahadhari zote zinzoelekezwa na wataalam wa afya dhidi ya ugonjwa wa corona kwa kuwakinga ni bora kuliko tiba.

Akiongelea changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini ambazo zilijikita katika kutoa huduma kwa jamii ikiwemo kodi kubwa, kodi za ardhi, umilikishwaji wa ardhi na makato ya ajira kucheleweshwa kwa ruzuku kutoka Serikalini, Rais Samia alisema kwamba amepokea changamoto hizo na yupo tayari kukaa na wataalam wake ili kuyapatia ufumbuzi na kuimarisha huduma hizo zinazotolewa na kanisa katoliki.

Naye,  KiongoziwaBaraza la Maaskofu Tanzania, AskofuMkuuwaJimboKatoliki Mbeya MhashamuGervasNyaisongaalisemakwambakanisalinaendeleakuwasaidiaWatanzaniakupambananaumasikinihasakatikakupataelimu bora pamojanahuduma bora zaafyaambaposhulenahospitalizakanisahilozinahudumiaWatanzaniawote.

“Lengo la Shulezetusiokufanyabiasharabalikutoahudumabilakujaliuwezowawazaziwanaotakakuelimishawatotowaokamailivyo Sera yaSerikaliyakoyaAwamuyaSita”, alisemaAskofuNyaisonga.

Kanisakatolikinchinipamojanahudumazakiroholakini pia linaendeshahudumambalimbaliikiwanipamojanakutoahudimazaafyanaelimuambapohadihivisasalinamilikishulezaawalihadisekondarizipatazo 754,hospitalipamojanavituovyaafyatakribani 464, ambapoasilimia 80 yahudumahizozimewekwaVijijinisehemuambazouhitajinimkubwazaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.