Habari za Punde

SMZ Yatarajiwa Kukabidhiwa Chanjo Laki Moja Kutoka Serikali ya China Hivi Karibuni.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akikabidhiuwa stakabadhi ya makabidhiano ya msaada wa Chanjo ya Covid-19 na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China  Anayefanyia Kazi zake Zanzibar Bw. Zhang Zhisheng, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Makamu Vuga Jijini Zanzibar. baada ya kuwasili ya kuwasili Zanzibar hivi karibuni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Bw. Zhang Zhisheng, wakati wa hafla ya kukabidhi stakabadhi ya Chanjo ya Covid-19, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Makamu Vuga Jijini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia Kazi zake Zanzibar Bw. Zhang Zhisheng, wakati wa hafla ya kukabidhi stakabadhi ya Chanjo ya Covid-19, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Makamu Vuga Jijini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimshkuru Balozo mdogo wa China aliefika Afisini kwake Vuga kwa ajili kumkabidhi Stakabadi za msaada wa Chanjo zilizotolewa na Nchi Hiyo ya China.


Na.Kassim Abdi.OMPR.

Jumla ya chanjo laki moja (100,000) zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya watu wa China.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar wakati akipokea Stakabadhi ya msaada huo wa chanjo kutoka kwa Balozi Mdogo wa China anaefanyia kazi zake Zanzibar Bwana Zhang Zhisheng

Mhe. Hemed alisema chanjo hizo aina ya SINOVAC zinategemewa kuwasili Zanzibar ndani ya muda mfupi baada ya kupokea Stakabadhi na mara baada ya kuwasili Zanzibar zinatakibidhiwa kwa Wizara ya Afya ikiwa ndio wizara yenye dhamana na musuala ya Afya.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itapokea chanjo hizo, ikiwa ni katika juhudi za kujikinga na Maradhi ya Covid 19, kwa lengo la kuwakinga wananchi wake kutokana na virusi vinavyosababisha maradhi hayo.

Akizungumzia Ubora wa chanjo hiyo Makamu wa Pili wa Rais aliwahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa chanjo hiyo ni salama kwani imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya matumizi.

Katika hatua nyengine Mhe. Hemed aliendelea kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuendelea kuunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa katika Sekta ya Afya, akitolea mfano misaada mbali mbali inayotolewa na Nchi hiyo katika Hospitali na Mnazi Mmoja na ya Hospital ya Abdallah Mzee kwa Upande wa Pemba.

Alifafanua kuwa, mashirikiano hayo yanaonesha ukaribu na udugu kati ya nchi hizo mbili yaliyoasisiwa kwa muda mrefu sasa ambapo hadi sasa China na Zanzibar zinashirikiana kupitia sekta tofauti.

Nae Balozi Mdogo wa China Bwana Zhang Zhisheng alisema China imejipanga kutoa chanjo ili kusaidia kinga dhidi ya covid 19 na alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa chanjo hizo ni salama kutokana na kupatikana kwa ruhusa ya kimatumizi kutoka  Shirika la Afya Duniani (WHO).

Aidha, Bwana Zhang Zhisheng alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Nchi ya China itaendeleza mashirikiano yaliyopo baina yao ili kuisaidia  Zanzibar kukuza uchumi wake ambapo serikali ya Jamuhuri ya watu wa China imejipanga kuisaidia Zanzibar katika kuwekeza kwenye Sekta ya Viwanda jambo ambalo litasadia kuinua uchumi wa zanzibar na watu wake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.