Habari za Punde

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazurui Azindua Chanjo ya Shindano ya Covid-19.

 Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akipiga sindano ya chanjo ya COVID 19 aina ya Cinovac katika uzinduzi wa chanjo hiyo uliofanyika Kituo cha Afya Lumumba Mjini Zanzibar.

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na wandishi wa Habari baada ya kupigwa sindano ya chanjo ya Covid -19.


Picha na Makame Mshenga.

Na Khadija KhamIs  - Maelezo,  22/07/2021 .                                                                                       

Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, alizindua na kuchanjwa chanjo COVID 19 aina ya Cinovac kutoka nchini China .

Amesema kuwa Chanjo hiyo ni hiyari ambayo iko salama na haina madhara kwa jamii  imethibitishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) .

Waziri Mazrui alieleza kuwa Chanjo hiyo inatolewa bila ya malipo kwa anaetaka kinga hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.