Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla Ajumuika na Wananchi Katika Sala ya Ijumaa Masjid Fattima Chuwini Wilaya ya Magharibi "A" Unguja.

Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdalla akiwakumbusha wananchi kuendelea kumuunga Mkono Rais Dk. Mwinyi katika kusimamia Uwadilifu wakati alipokuwa akiwawasalimia waumini waliotekeleza ibada ya sala ya Ijuma katika Masjid Fatiima uliopo Chuini.

Na.Kassim Abdi OMPR, Zanzibar.                                                                                                             

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.Hussein Mwinyi katika kusimamia haki za watu wanyonge kwa kusimamia uwadilifu.

Mhe. Hemed alieleza hayo wakati akiwasalimia waumini na wakaazi wa Chuini mara baada ya kutekeleza ibada ya sala ya Ijumaa katika Masjid Fatiima chuwini Wilaya ya Magharibi”A”Unguja

Alisema kuwa, kuna kila sababu kwa waumini na wananchi kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais kutokana na dhamira njema alionayo ya kuwatumikia wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba.

Makamu wa Pili asisitiza kwamba suala la uwadilifu  utekelezaji wake ni jambo la lazima na wala sio jambo la hiyari hivyo, aliwaomba waumini hao kila mmoja kutekeleza jambo hilo kwa nafasi aliyo kuwa nayo.

“Rais wetu ni muuminu mkubwa wa suala la uwadilifu sisi wasaidizi wake kila siku anatuhimiza juu ya jambo hilo “Alisema Mhe.Hemed.

Alifahamisha kuwa serikali imekuwa ikipata changamoto kubwa kwa wafanyabiashara kukosa uwadilifu katika biashara zao kwa kukwepa kulipa kodi inayostahiki kwa kufanya njia udanganyifu juu ya mizigo wanayopisha katika milango mikuu ya ukusanyaji wa kodi.

Aliwataka wananchi kufahamu dhamira ya Mhe. Rais ya kufanya mabadiliko kupitia teuzi zake kwani hana nia ya kumkomoa mtu bali anachohitaji ni kuweka watu wanaoweza kusimamia uwadilifu na kuwatumikia wananchi.

Akizungumzia juu ya suala zima la maradhi ya Covid – 19 Makamu wa wa Pili aliwakumbusha waumini hao kuendelea kuchukua tayadhari na kufuata maelekezo yanayotolewa na watalamu wa masuala ya Afya ili kujilinda na maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa huo.

Alisema wimbi la tatu lililotabariwa na watalamu dalili zake zimeanza kuonekana akitolea mfano Nchi ya Uganda ambayo wananchi wake waliekewa Karantini kwa kipindi cha siku Arubaini kubaki majumbani bila kutoka nje.

Aliwakumbusha wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kutmia njia ya kuepuka mikusanyiko isiokuwa na lazima, kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka, kunawa kila baada ya muda kwa kutumia vitakasa mikono(Hand Sanitaizer).

Pia, Makamu wa Pili wa Rais aliwataka waumini waliosali katika mskiti huo na wananchi wote kwa ujumla kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya katika maeneo yao wanayoishi kutokana na athari kubwa juu ya vijana ambao ni tegemeo la taifa.

Alieleza kuwa, serikali imejipanga vyema kukabiliana na wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uwingizaji na usambazaji wa madawa ya kulevya kwa kudhibiti mianya inayotumiwa kupitisha dawa hizo.

"Vitendo hivi havijengi nchi yetu bali vinaharibu vijana wetu"Alieleza Makamu wa Pili.

Nae, Khatibu aliehutubu katika mskiti huo Sheikh Twalib Abdalla Twalibu alisema jamii inafurahishwa sana na jitihada zinazochukuliwa na Mhe. Rais wa Zanzibar Dk. Huseein Mwinyi na wasaidizi wake katika kurejesha mali za wananchi wanyonge zilizokuwa zimezoporwa na watumishi wasiokuwa waaminifu.

Sheikh Twalib aliwataka watumishi waliokabidhiwa dhamana za kuwatumikia wananchi kuwa waadilifu na kutenda haki na kuachana na tabia ya kupora mali za Umma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.