. Msanii Nandy akitumbuiza leo Julai 2,2021 kwenye sherehe ya ufungaji wa UMISSETA 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Msanii Mr Bluu akitumbuiza leo Julai 2,2021 kwenye sherehe ya ufungaji wa UMISSETA 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara
a. Msanii Sholo Mwamba akitumbuiza leo Julai 2,2021 kwenye sherehe ya ufungaji wa UMISSETA 2021 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
a. Waziri bashungwa akiwa na Katibu Mkuu wake Dkt. Hassan Abbasi, viongozi na wachezaji wa timu za mpira wa miguu kwenye fainali baina ya timu ya Pemba na Mtwara ambapo Pemba wameibuka washindi baada ya kuiadhibu mtwara mabao 2-0.
a. Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akitoa maneno ya kumkaribisha Mhe. Bashungwa leo Julai 2,2021 ili atoe hotuba ya ufungaji wa UMISSETA 2021
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akihutubia leo Julai 2,2021 kwenye ufungaji wa UMISSETA mjini mtwara.
Na John Mapepele, Mtwara
Serikali imesema ipo kwenye hatua za mwisho za kuanzisha
shule maalum za michezo, za msingi na sekondari, katika mikoa yote nchini lengo
likiwa ni kuwa na shule na vituo maalum vya kuendelezea vipaji vya michezo (sports academies).
Akizungumza kwenye Sherehe za kufunga mashindano ya
Michezo na Taaluma kwa Shule za Sekondari(UMISSETA) mjini Mtwara leo Julai 2,2021 Waziri wa
Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amese Shule hizi zitakuwa zinalea na
kuendeleza vipaji vya michezo mbalimbali, na Serikali itakuwa inasimamia kwa
ukaribu, kuhakiksiha kuwa vituo vya michezo vya shule za msingi na sekondari,
vinapatiwa mahitaji muhimu yatakayo saidia katika kuendeleza vipaji hivyo.
Amesema Serikali kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo –
Malya, inaanzisha kituo maalum cha michezo cha kuendeleza vipaji (Centre of Sports Excellency),
vitakavyokuwa vinapatikana kutokana na mashindano haya, na maeneo mengine
mbalimbali nchini.
« Chuo cha maendeleo ya michezo Malya kimeanzisha
mafunzo ya astashahada, ili kupanua wigo wa wanufaika wake, pia kimefungua
kituo cha mafunzo Dar es salaam na Ruvuma, ili kusogeza huduma kwa wananchi
wengi zaidi. Ni matumaini yetu kuwa, kupitia Chuo hiki, tutaweza kupunguza
pengo la watalaam, na walimu wa Michezo ambalo tunalo hivi sasa »
amesisitiza Mhe. Bashungwa
Katika mashindano ya mwaka huu ya UMISSETA mkoa wa Dar es
Salaam umeibuka mshindi wa kwanza wa
jumla katika michezo yote.
Pia amememshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Hassan Suluhu, kwa maelekezo
yake ya kuondoa kodi ya VAT, katika kununua na kuingiza nyasi bandia nchini,
ili tuweze kujenga na kukarabati miundombinu yetu ya michezo.
« Wizara
yangu imejipanga kuanza kuhamasisha taasisi na wadau mbalimbali, kuchangamikia
fursa iliotolewa kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vyao. Nimatumaini yetu
kuwa, kwa hatua hii tunakwenda kuimarisha, na kuboresha mioundombinu ya michezo
nchini » amefafanua Mhe. Bashungwa.
Ameongeza kuwa, Mhe. Rais kupitia bunge la bajeti
lililoisha mwezi Juni, 2021, ameruhusu asilimia 5 kutoka kwenye michezo ya
kubashiri (sport betting), kuingia
kwenye mfuko wa maendeleo ya michezo, unaosimamiwa na Baraza la Michezo
Tanzania (BMT), ili fedha hizo ziweze kutumika kwa ajili ya maendeleo ya
Michezo.
Amesema kutunishwa kwa mfuko huo kutatoa fursa ya
kuendeleza michezo mbalimbali nchini, kwa ngazi zote, ikiwemo mashindano ya
UMITASHUMTA na UMISETA.
Amemhakikishia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Majaliwa
utekelezaji wa maagizo mbalimbali, ya kuhakikisha Wizara yake inaweka mikakati
mbalimbali ya kuendeleza michezo nchini ambayo aliyatoa wakati wa ufunguzi
wa UMITASHUMTA hivi
karibuni ambapo amesema baadhi ya maelekezo tayari yameshafanyiwa kazi.
Baadhi ya maelekezo hayo ni pamoja na, kufanya tahimini
ya Vyuo vya Elimu, vilivyokuwa vinafundisha michezo na sasa havifundishi; na
uanzishwaji wa shule maalum za michezo mikoani.
. « Kupitia ushirikiano na umoja wa Wizara zetu
maagizo haya na mengine tutayashughulikia kwa kasi na weledi, ili kuhakikisha
sekta ya michezo inakuwa nchini »
Aidha amesema Serikali kwa, kupitia Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo itazindua mpango mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya
Michezo mwezi Julai, 2021. Mpango mkakati huo umetoa muelekeo wa jinsi ya
kuendesha michezo, kwa kuzingatia maelekezo mbalimbali yaliotolewa kwenye Ilani
ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, ambapo pamoja na mambo mengine, mpango huo
unaweka mkakati wa jinsi ya kuingia kwenye michezo ya kulipwa, ili kuwapatia
vijana ajira kwa kutumia vipaji vyao, na kujipatia vipato wao binafsi lakini
pia kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya michezo. Kama Waziri mwenye
dhamana, nitahakikisha kwamba tunafikia malengo hayo na kazi inaendelea.
Pia ametumia muda huo kuwashukuru wasanii wa kizazi kipya
waliokuwa wakitoa burudani katika kipindi chote cha UMITASHUMTA na UMISSETA
ambao wameleta hamasa kubwa na burudani kwa wanamichezo na wadau
mbalimbali walioshiriki mashindano ya
mwaka huu.
Miongoni mwa
wasani wa kizazi kipya waliotoa burudani kwenye ufungaji wa UMISSETA leo
Julai 2,2021 na kuteka mji wa mtwara
na viunga vyake ni pamoja na Maarifa,
Kala Jermiah, G-Nako, Mr Blue, Shishi, Nandy na Sholo Mwamba.
“Asanteni
sana kwa ushirikiano wenu mkubwa, pamoja na burudani mlioionesha, na mtakayo
endelea kuifanya hapa leo, ili kutoa burudani ya kuhitimisha michezo hii. Kwa
hakika wana Mtwara wamefurahi na kuburudika sana. Michezo sasa ni ajira, hivyo
kwa kuendeleza michezo hii, ni kuaandaa eneo muhimu litakalowapatia vijana wetu
ajira kupitia vipaji walivyonavyo” amesisitiza Bashungwa
Naye Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo,
Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara
ya habari itaendelea
kusimamia sera na kuweka mikakati madhubuti ili kuinua maendeleo ya
wasanii nchini.
No comments:
Post a Comment