Habari za Punde

Uzinduzi wa msimu wa manunuzi ya karafuu mwaka 2021/2022 bandarini Wete.

MENEJA Masoko Zantel Zanzibar Rukia Iddi Mtingwa, akisoma taarifa ya ushirikiano baina ya Kampuni ya Zantel na shirika la ZSTC, ili kutoa huduma ya malipo ya wakulima wa karafuu kwa njia ya Ezypesa, wakati wa uzinduzi wa msimu wa mpya wa manunuzi wa zao la karafuu, hafla iliyofanyika Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

BAADHI ya wafanyakazi wa kituo cha ununuzi wa zao la karafuu bandarini Wete, wakisafisa baadhi ya karafuu ambazo zimefikishwa kituoni hapo, kabla ya kununuliwa na shirika la ZSTC katika msimu mpya wa zao hilo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

Afisa mkuu wa fedha Zantel Azizi Said Ali wapili kushoto na Mkuu wa mauzo na Usambazaji Zantel Emamanuel Joshua, wakipatiwa maeleo juu ya utafauti wa karafuu za gredi ya kwanza na gredi ya pili, kutoka kwa wafanyakazi wa shirika la ZSTC Bandarini Wete, wakati wa uzinduzi wa msimu wa manunuzi wa zao hilo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

WAZIRI wa Biashara  na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar  Omar Siad Shaaban, (kushoto) akimsikiliza kwa makini Afisa Mkuu wa Fedha Zantel Zanzibar Azizi Said Ali (mwenye maiki), juu ya mikakati yao ya ulipaji wa fedha kwa mfumo wa Ezypesa kwa wakulima wa zao la karafuu, wakati wa uzinduzi wa msimu wa manunuzi ya karafuu huko Bandarini Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MENEJA Masoko Zantel Zanzibar Rukia Iddi Mtingwa, akiwaeleza jambo watendaji wa Zantel akiwemo Afisa Mkuu wa Fedha Zantel Azizi Said Ali na Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Zantel Emmanuel Joshua, mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa msimu wa manunuzi ya karafuu mwaka 2021/2022 huko bandarini Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.