Habari za Punde

Wanafunzi wa Shule za Sekondari Tanga Waonyesha Ubunifu Mkubwa Maonesho ya Sayansi.

Kaimu Katibu Tawala Upande wa Elimu Mkoa wa Tanga na Zalia Gaula akizungumza wakati wa Maonyesho ya Sayansi kwa Vijana wa Shule za Sekondari Mkoani Tanga yamefanyika kwa mara ya kwanza katika shule ya Sekondari Tanga School
                                         Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja

Na.Assenga Oscar   

MAONYESHO ya Sayansi kwa Vijana wa Shule za Sekondari Mkoani Tanga yamefanyika kwa mara ya kwanza huku wanafunzi wakionyesha ubunifu mbalimbali na kuweza kusaidia kupambana na changamoto zilizopo kwenye ulimwengu wa sasa kwa kutumia Teknolojia na Sayansi.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ,Mratibu wa maonyesho hayo ya Sayansi kwa wanafunzi wa shule za Sekondari Mkoa wa Tanga Mwalimu Nelson Makundi alisema lengo kubwa la la maonyesho hayo ni kutumia Sayansi na Teknolojia kuibadili Tanzania ya sasa


Alisema kutokana na kwamba sayansi ikitumika vizuri inaweza kuwa chachu ya kuweza kufikia maendeleo makubwa kutokana na kwamba hata viwanda ambavyo vitaanzishwa vitahitaji wataalamu ambao wataweza kufanya shughuli kwenye maeneo hayo.


“Nitoe wito kwa Serikali kwani maonyesho hayo yamekuwa yakifadhiliwa na wafadhili mbalimbali lakini walikuwa wanatama sana wao nao wawaunge mkono  kwa sababu Taifa linategemea sana sayansi kwa maendeleo”Alisema


Hata hivyo alisema upo umuhimu wa Serikali kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na wanasayansi na vijana hao ili kuweza kufanikisha malengo kwa Taifa na kuifanya Tanzania kuwa sehemu nzuri ya kuishi.


Awali akizungumza wakati wa maonyesho hayo Kaimu Katibu Tawala Upande wa Elimu Mkoa wa Tanga na Zalia Gaula alimpongeza Mkuu wa Shule ya Sekondari Tanga School Andrew Mwakanyamale kwa kupatia nafasi ya kuweza kuandaa mashindano hayo ambayo yamefanikiwa sana ikiwemo walimu ambao walijitoa pamoja na vipindi vya kawaida kuweza kuwasaidia wanafunzi hao.


Alisema amepitia kwenye maonyesho hayo ni mazuri kutokana na kila mwanafunzi kuwefanya kazi nzuri sana huku akiwataka kuhakikisha wanapokuwa madarasani wana kuwa makini kusikiliza walimu wenu wanachokifundisha ili waweze kukitumia kwenye kupata ufaulu.


“Mwanasayansi mkubwa anaanzia kwenye maonyesho kama hayo hivi sasa Tanzania tumeingia kwenye uchumi wa Kati wa viwanda ambapo tunahitaji wanasayansi na wanasayansi wanatengenezwa hivyo sisi  kama mkoa tunaouwezo wa kuwaandaa wanayansi baadae wakawa na mchango mkubwa kwenye Taifa ”Alisema


Alisema pia amefurahishwa na kifaa cha kuzuia mawasiliano kwa sababu kama mwanafunzi anatumia simu bwenini inamzuia hivyo wamefanya kitu kizuri kutokana na kwamba  shule nyingi zinaunga moto lakini wanasema chanzo hakujiukalani lakini tatizo kubwa ni njia za kuchaji simu ambapo wanafunzi wanatafuta sehemu ya kuchagi simu ivyo wanaunganisha nyaja bila kuwa na ujuzi.


Afisa Elimu Taaluma hiyo alisema hatua hiyo inapelekea mabweni kushika moto na hivyo ni kuzuri huku akitaka nitakapoanza kufanya kazi ni vizuri kianze kutumika kwenye shule hiyo .


Hata hivyo aliwashauri wakuu wa shule,walimu na  walezi wapate muda ya kukaa na wanafunzi wenye changamoto za kujirudia mara kwa mara kwani makosa hayo ndio yanasababisha wasifanye vziuri darasani hivyo wanaweza kukuta wanafunzi wenye matatizo ya kifamilia.


Alisema hivyo ni muhimu kuona namna nzuri ya kuwasaidia ili kuweza kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hao ikiwemo kueleza kuvutiwa na maonyesho hayo kwa sababu wametumia dhana na vifaa vinavypatikana kwenye maziingira ya hapa nchini.


“Lakini natamani siku moja kwa hicho wanachofanya wanafuzi wanaweza kutafuta chanzo cha kufanya njia mbadala ya asili ya kutumia mmea au kitu ambacho kitaweza kutumika kufukukuza mbu waonekeza malaria maana ugonjwa huo ni hatari”Alisema


Kwa upande wake Afisa Elimu Upande wa Sekondar Jiji la Tanga Lusajo Gwakisa alisifu juhudi ambazo zimeonyeshwa kwenye uandaaji wa maonyesho hayo huku akitoa ombi lake kwa wanafunzi wa sayansi na masomo mwengine kuendelea kujitahidi na kuzingatia wanayofundishwa walimu.


“Kwa maana wanajitahidi nimefurahi kuona watoto wanajua kufanya utafiti na kukusanya data na kufanya uchambuzi wa data na kilichoni furahisha ni ubunifu mkubwa mliokuwa mkiunyesha niwaombe wote mjitahidi mfike Chuo Kikuu”Alisema


Hata hivyo alisema angeomba wale ambao wamejitahidi kuendelea kufanya vizuri na wao kama Halmashauri  Idara ya Elimu sekondari watawasaidia mazoezi yote yalikuwa yakiendeshwa kwa kukosa vifaa na masuala mengine kwa wale wote waliofanya wataboresha zaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.