Habari za Punde

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo atembelea miradi ya maendeleo Wilaya za Kaskazini A na B na kuelezea kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa

Katibu mkuu Wizara ya habari, vijana, Utamaduni na michezo Fatma Hamad Rajab  akionesha hisia za kukerwa na harakati za miradi ya kimaendeleo zilivyoendeshwa bila ya utaalamu na kuisababishia hasara serikali

 
Katibu mkuu Wizara ya habari, vijana, Utamaduni na michezo Fatma Hamad Rajab akisisitiza jambo wakati alipokuwa katika ziara ya kutembelea miradi kulia ni Mkuu wa jeshi la kujenga uchumi Zanzibar JKU Captain Makame Abdalla Daima

Na Mwandishi wetu

Katibu mkuu Wizara ya habari, vijana, Utamaduni na michezo Fatma Hamad Rajab amesema hajaridhishwa na miradi ya maendeleo Wilaya ya Kaskazini 'A' na 'b' kutokana na waliofanya kazi za uchimbaji visima sio wataalamu. 

Akizungumza katika ziara ya kuangalia miradi ya maendeleo ya baraza la vijana Wilaya hizo, alisema kutokana na changamoto hiyo imepelekea kuitia hasara Serikali pamoja na kudumaza maendeleo ya vijana. 


Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Zanzibar Salum Issa Ameir amesema hatomvumilia mtendaji yeyote anaepewa dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo ya vijana kwa lengo la kuzorotesha maendeleo yao. 


Mkuu wa jeshi la kujenga uchumi Zanzibar JKU Captain Makame Abdalla Daima amesema hali ya miradi sio nzuri hivyo ni vyema uongozi wa Wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo pamoja na uongozi wa JKU kukaa pamoja ili vijana kuendelea na harakati za maendeleo wanazozifanya


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.