Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe.Mwanaidi Ahimiza Halmashauri Nchini Kutenga Mikopo Kwa Wanawake.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akikabidhi malighafi ya kutengeza vikapu kwa Kikundi cha Wanawake wajasirimali cha Malkia wa Nguvu kilichopo Manispaa ya Songea mkoani Songea.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wanakikundi cha  Mkombozi Peramiho Mkoani Ruvuma alipokitembelea Kikundi hicho.

Na Mwandishi Wetu Songea

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Mwanaidi Ali Khamis amezitaka Halmashauri nchini kutekeleza kikamilifu matakwa ya ya kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani  kwa ajili mikopo kwa Wanawake, Vijana na wenye ulemavu katika Halmashauri husika.

 

Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake  kukagua shughuli za mbalimbali zinazolenga kuwawezesha makundi hayo katika jamii likiwemo suala la mikopo kwa wanawake Mkoani humo.

 

Mhe. Mwanaidi amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuendelea kutoa elimu kwa kuwahamasisha Wanawake ili waweze kujiunga katika vikundi vya kiuchumi ili iwe rahisi kwa serikali kuwapatia huduma mbalimbali ikiwemo mikopo inayotolewa kupitia halmashauri.

 

"Maafisa Maendeleo ya Jamii jipangeni kuweni wabunifu wahamasisheni Wananawake kujiunga katika vikundi vya kiuchumi Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuwawezesha wananchi hasa Wanawake kujikwamua kiuchumi" alisema Mhe. Mwanaidi

 

Kwa upande wao Wananchama wa Kikundi cha Malkia wa Nguvu kilichopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Stella James Ambano ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha kupata mikopo kutoka katika Halmashauri na hivyo kuweza kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa urahisi.

 

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Mwanaidi amekitembeela Kikundi cha Wanawake Wajasirimali cha Ukombozi Peramiho kinachojishughulisha na utengezaji wa sabuni na ufumaji wa mashuka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.