Habari za Punde

WATAKAO KATISHA MASOMO WATOTO WAKIKE KUKIONA

Na Lucas Raphael,Tabora

Serikali imesisitiza kwamba itaendelea kuwekeza kwenye elimu ya mtoto wa kike  na wale wote watakaothubutu kukatisha masomo kwa kuwapa mimba hataweze kukwepa na kifungo cha miaka 30 jela.

Kauli hiyo imetolewa leo na waziri kuu Kassimu Majaliwa alipokuwa Akikangua miundombinu ya shule za kongwe za serikali za  sekandari ya Tabora Walavuna na Tabora Wasichana mkoani hapa.

Alisema kwamba serikali inakusudia kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye elimu ya mtoto wa kike kuanzia kwenye miundombinu ya mabweni madarasa ili kuweza kutimiza ndoto zao.

“serikali hii itakubali kitendo chochote cha mtu wa aina yoyote kukatisha mtoto wa kike masomo na kumuacha akirandaranda mitaani bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria  jambo hilo halikubaliki “alisema waziri mkuu.

“Lazima ndoto wa wa watoto wa kike zitimie kwa kuwapa elimu iliyobora kwa kujenga majengo bora, maabara zuri na vyumba vizuri vya madarasa kwa ajili ya kusomea na  kutiza ndoto zenu “alisema.

Alisema kwamba  serikali ya awamu ya sita imedhamiria kumsomesha mtoto kuanzia chekechea hadi kidato cha nne na kuendelea chuo kikuu ili kuweza kutimiza ndoto zao za mafanikio hasa ya kielimu na maisha kwa ujumla.

Alisema kwamba serikali ya  mama Samia Suluhu Hassani imetoa fedha zaidi ya bilioni ya fedha kwa ajili ya kuwekeza katika mazingira mazuri kwa ajili ya mtoto wa kitanzania kuweza kupata elimu bora.

Alisema kwamba serikali ilitoe bilioni 2.2  kwa ajili ya kufanyia ukarabati wa miundumbinu ya majengo ya shule zote kongwe ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia .

Hata hivyo alisema kwamba serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 7 kwa ajili ya ujenzi  wa vyumba vya madarasa 590 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani .

Alisema kwamba serikali imefanya hivyo ili kusaidiana na halmashauri za wilaya nchini kuweza kukamilisha vyumba hivyo kwa wakati na kuondoa usumbufu kwa watoto watakaojiunga na elimu ya sekondari mwakani.

Majaliwa aliendelea kusema kwamba kutokana na hali hiyo serikali na wananchi waone umuhimu wa kodi mbalimbali ambazo wananchi wanatoa kwa ajili ya serikali  na jukumu kubwa la serikali ni  kuwapelekea  maendelea wananchi.

Awalimu mkuu wa mkuu wa shule ya Tabora Wavulana Deogratias Mwambuzi alimweleza waziri mkuu Kassim Majaliwa kwamba hadi kufikia sasa mabweni hayo yametumia kiasi cha shilingi milioni 433.5 kwa ajili ya ukarabati miundumbinu  hiyo.

Alisema kwamba hitaji la kuboresha miundombinu ya mazingira ya shule hiyo ambayo serikali ilitoa kisiasi cha shilingi milioni 500 kupitia Mamlaka ya elimu Tanzania TEA.

Alisema kwamba  fedha hizo zilikarabati mabweni 5 ambayo ni Bweni la Kimweli ,Ruhinda, Milambo,Mkwawa  ,Kilimo na ukarabati wa maktaba ya shule hiyo.

Naye makamu mkuu wa shule ya Tabora wasichana Avidia Nshunju alimweleza waziri mkuu wanaipongeza serikali kwa mradi wa ukarabati mkubwa ambao umewawezesha kupunguza changamoto ya milipuko ya umeme katika majengo yaliyokarabatiwa na pia imesaidia wanafunzi kujisomea wakiwa mabwenini badala uya kutengemea madarasani tu ambako miundombinu yake ni chakavu.

Aidha aliomba  kuwaongezewa  mradi wa ukarabati wa majengo ambayo yamekuwa ni chakavu na kupelekea gharama kubwa za matumizi ya umeme na maji .

Alisema kubwa waliyokuwa nayo ni kuwaongezea ukarabati wa Bwalo la Chakula na Jiko,Maabara ,jingo la Utawala ,Madarasa,Mabweni 9 ,ujenzi wa maabara ya Cumputa (ICS) na ujnzi wa Maktaba mpya ya shule.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.