Habari za Punde

ASA Waaza Kusambaza Mbegu kwa Wakulima.

Baadhi ya magari ya mizigo ya wakala wa mbegu bora asa yakiwa yanapakiza mbegu kupeleka katika shirika la reli kwa aajili ya kusafirisha mbegu hizo kuelekea mkoa wa tabora na mwanza.

Lucas Raphael,Morogoro 

Na Lucas Raphael,Morogoro.

Wakala wa Mbegu bora za kilimo Nchini(ASA) wameanza kusambaza mbegu bora za kilimo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwa msimu wa mwaka 2021/2022 kupitia usafiri wa shirika la Reli Nchini(T R C).

Akizungumza na waandishi wa Habari jana katika kituo cha Reli mkoani Morogoro Kaimu meneja Masoko wa wakala wa Mbegu za kilimo Nchini Edward Mugi alisema ni mara ya kwanza Taasisi hiyo kuanza kusafirisha mbegu kupitia Shirika la Reli kutokana na usalama na mabadiliko yaliyowekwa.

Alisema Uongozi wa Taasisi hiyo ulifikia maamuzi ya kuanza kusafirisha mbegu hizo kwa njia ya Reli hasa katika mikoa inakopita  Reli hiyo lengo ni kuwafikia wakulima kwa haraka na usalama zaidi kutokana na umuhimu wake.

Alisema Usafiri huo unapunguzo kubwa la fedha tofauti na usafiri wa barabara hali inayosaidia kupunguza gharama za matumizi.

Alisema uongozi wa Reli umetoa mabehewa mawili ya mizigo kwa Taasisi hiyo muhimu serikalini na kuongeza kuwa bei za mbegu  zitapungua tofauti na makampuni mengine yanayouza mbegu kwa bei ya juu.

Aliwataka wakulima kuchangamkia mbegu hizo zinazipoanza kusambazwa mapema ilikuwahi msimu wa kilimo nakuongeza kuwa mbegu hizo zimehakikiwa na kuthibitishwa na taasisi za serikali kuwa zinatija kwa wakulima.

Mkuu wa Shirika la Reli Mkoa wa Morogoro Salvatory  Kimaro alisema kwa sasa wameanza kupokea wateja wengi wanaotumia usafiri huo kutokana na maboresho yaliyofanywa na shirika.

Alisema baada ya kuona Wakala wa Mbegu bora za kilimo kuweka nia ya kusafirisha mbegu zao kwa usafiri wa Reli taratibu zilifanyika haraka ili wateja hao waweze kupata huduma bora.

Alisema usafiri wa Reli umeboreshwa kuanzia miundombinu ya barabara,mabehewa sambamba na ulinzi wakutosha kwa kutumia jeshi la polisi lengo ni kuhakikisha mizigo ya wateja inafika kwa usalama.

Alisema mzigo wa kwanza unaosafirishwa ni Tani 80 sawa na mabehewa mawili huku akiwaahidi mzigo huyo utafika salama.

Kimaro alitoa wito kwa taasisi nyingine za serikali na zile zisizo za kiserikali kuliamini shirika hilo katika kutumia usafiri wa reli ili mizigo yao ifike mapema na kwa usalama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyakazi wanao pakiza mizigo na kushusha mizigo wamepongeza kuona Taasisi za serikali kuanza kutumia shirika hilo kwa kusafirisha mizigo yao.

Zamos Adriani mbeba mizigo mkoani Morogoro alisema kwa sasa wameanza kufanya kazi nyingi kupitia Taasisi za serikali zinazo safirisha mizigo kupitia Reli ya kati.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.