Habari za Punde

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mlezi wa CCM Mkoa wa Tanga Mhe Hemed Suleiman Aendelea na Ziara yake ya Kichama Mkoa wa Tanga.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimakabidhi Cheti na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga kwa kazi nzuri inayondelea kufanya na viongozi wa Chama wa Mkoa huo katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Na.Kassim Abdi OMPR.

Viongozi wa Chama na serikali wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuchukua hatua za haraka katika kuzuwia matumizi mabaya ya Fedha za watanzania ili kujenga nidhamu kwa watumishi wake.

Mlezi wa Mkoa wa Tanga ambae pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alitoa agizo hilo wakati akizungumza na viongozi Pamoja na wanachama wa wilaya ya Handeni katika Ukumbi wa Mikutano wa Makuti uliopo Handeni Mjini.

Mjumbe huyo wa Kamati kuu ya CCM Taifa alisema akiwa mlezi wa Mkoa wa huo kichama atahakikisha Mkoa wa Tanga unakua mfano kwa matumizi ya fedha za serikali zinazolenga kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Katika kulitekeleza hilo Mhe. Makamu wa Pili wa Rais alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kuwachukulia hatua watendaji wake wasiokuwa waaminifu kwa lengo la kuhakikisha ilani CCM inatekelezwa Vyema.

Akizungumza katika kikao hicho cha ndani Mhe. Hemed aliwakumbusha viongozi hao kuachana na tabia ya makundi kupitia uchaguzi uliomalizika mwaka 2020 ili kuwapa fursa viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kuwatumikia wanachi katika maeneo yao.

Mapema asbuhi mjumbe huyo wa kamati kuu alitembelea shina nambari tano kata ya kivesa wilaya ya Handeni na kusalimiana na Wanachama.

Akiwa katika eneo hilo viongozi mbali mbali akiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Handeni walimuleza mlezi huyo juu ya Faraja yao kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania kwa kutoa kiasi kikubwa cha  Fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Handeni.

Wakati wa Mchana Makamu wa Pili wa Rais alishiriki katika ujenzi wa kituo cha Afya Sendeni ambapo kituo hicho kitakapokamilika kinatarajiwa kuwahudumia wananchi takribani Laki Tatu wa wilaya ya handeni.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo mganga mkuu wa Afya Wilaya KANASIA MICHEL SHOO  alimueleza Makamu wa Pili wa Rais Faraja waliohi nayo wananchi wa Handeni kwa Rais Samia kwa kutenga Shillingi Milioni 250 fedha ambazo zimetokana na TOZO za wananchi zitokanazo na miamala ya simu za mkononi.

Wakati wa Jioni Mhe. Hemed alikfika katika wilaya ya Korogwe katika eneo la skuli ya Sekondari ya  JOEL BENDERA na kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa maabara Pamoja na ufungua vyumba viwili vya madarasa ya kusomea wanafunzi.

Akikagua mradi huo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu aliwaagiza wasimamizi wa ujenzi huo kufanya baadhi ya marekebisho kwa madawati ili kutoa huduma nzuri kwa wananfunzi wa Skuli hiyo.

Ziara hiyo ya Mlezi wa Mkoa wa Tanga inatarajiwa kuendelea kesho katika wilaya ya Korogwe na Wilaya ya Muheza ambapo Mhe. Hemed atetembelea miradi mbali mbali ikiwemo miradi ya miundombinu ya Barabara.

Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya Sindeni akiwa katika muendelezo wa ziara yake katika Wilaya ya Handeni.
Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akishiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya Sindeni akiwa katika muendelezo wa ziara yake katika Wilaya ya Handeni.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa akipanda Mti mara baada ya kushiriki katika ujenzi wa Kituo cha Afya Sindeni katika wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.
Mhe. Hemed akifungua vyumba viwili vya madarasa ya kusomea wanafunzi katika skuli ya sekondari ya Joel Bendera iliopo wilaya ya Handeni katika muendelezo wa ziara katika Mkoa Tanga.
Mhe. Hemed akifungua vyumba viwili vya madarasa ya kusomea wanafunzi katika skuli ya sekondari ya Joel Bendera iliopo wilaya ya Handeni katika muendelezo wa ziara katika Mkoa Tanga.

Mlezi wa Mkoa wa Tanga Mhe. Hemed akisalimiana na wanachama Shina nambari Tano kata ya Kivesa wakati alipofika katika shina hilo kufuatia ziara yake katika Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.