MRATIBU
wa mradi wa ushirikishaji wanawake katika uongozi kutoka TAMWA ZNZ, Salma Amir
Lusangi akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari kutoka vyombo
mbali mbali Pemba, mafunzo hayo yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar Ofisi ya Pemba,
chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway nchini
KAIMU
meneja wa Radio Jamii Mkoani Said Omar Said, akiwasilisha majibu wa kundi namba
mbili wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari juu ya kuwajengea uwezo na
ufahamu, taratibu za ufuatiliaji wa matumizi ya mali za umma, ushawishi Pamoja
na utetezi wa masilahi ya umma, mafunzo yaliyofanyika Ofisi za TAMWA Zanzibar
Ofisi ya Pemba
MRATIB
wa TAMWA Pemba Fat-hiya Mussa Said, akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tatu
kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali Pemba, mafunzo hayo
yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar Ofisi ya Pemba, chini ya ufadhili wa Ubalozi wa
Norway nchini.
BAADHI ya waandishi wa habari kutoka Vyombo mbali mbali vya habari Pemba, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya siku tatu juu ya mradi wa ushirikishaji wanawake katika uongozi, mafunzo hayo yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar Ofisi ya Pemba, chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Norway nchini.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)
No comments:
Post a Comment