Habari za Punde

Waziri Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima Aitembelea Familia ya Mama Zaina Khamis Kata ya Bangula Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amemtembelea Mama Zaina Khamis mwenye Watoto sita waliokosa fursa ya kupata elimu ingali umri wao wanastahili kuendelea na masomo anaeishi na wanae katika kata ya Bangulo Gongo la mboto, Jijini Dar es Salaam.

Familia hiyo ilikuwa ikiishi Tabata Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam kabla ya kutelekezwa na kuamia Bangulo ili kupata hifadhi katika kipindi hiki wanachopitia hali ngumu ya maisha na changamoto ya uhusiano wa kifamilia. 

Akiongozana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam Dkt. Mfaume pamoja na Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Mkoa Dkt. Gwajima ameagiza familia hiyo kupewa hifadhi katika makazi ya kulelea Watoto wenye uhitaji, huku taratibu za kuwapeleka shule Watoto wote zikiendelea. 

Pia, amewaagiza Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii kufuatilia mzazi mwenza wa Mama Zaina ili kujua ukweli kuhusu jambo hilo ikibidi kutatua changamoto zao ili kuinusuru familia hiyo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.