Habari za Punde

kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani.

Na.Kassim Abdi OMPR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameuagiza uongozi wa Wizara ya Kilimo,Umwagiliaji, MaliasilI na Mifugo kuchukua jitihada za maksudi za kuimarisha uzalishaji wa chakula ili kuifanya Zanzibar iweze kujitegemea.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla alitoa agizo hilo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya chakula Duniani hafla ambayo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakili Kikwajuni Jijini Zanzibar.

 

Amesema kwa sasa hali sio ya kuridhisha katika suala zima la uzalishaji wa chakula jambo linalopeleka changamoto kwa Zanzibar kuingizwa kwa bidhaa zilizopitwa na wakati na kupelekea kuathiri Afya za Wananchi wake.

 

Mhe. Hemed alimuagiza Waziri ya kilimo kupitia wataalamu waliopo katika wizara hiyo kuutumia utaalamu wao kwa kuzalisha zaidi ili kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nje ya nchi na pale zinapotokea changamoto zinazowakabili wasisite kuziwasilisha serikalini.

 

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais aliishauri Jamii  kufuata kanuni bora za ulaji wa chakula utakaowasaidia kuimarisha afya zao ili kupunguza tatizo la lishe Nchini.

 

Alieleza kuwa,Maadhimisho hayo yanalengo la kuhamasisha watu hususan wanaoishi Vijijini na wale walio katika mazingira magumu,kushiriki katika kufanya maamuzi sahihi juu ya ulaji bora wa chakula.

 

Makamu wa Pili wa Rasi alibainisha kwamba,Takwimu za hali yali ya chakula Zanzibar zinaonesha kuwa uzalilishaji na upatikanaji wa chakula unaendelea kuimarika ukilinganishwa na mahitaji halisi ya mwaka hadi mwaka.

 

Alisema Zanzibar inategemea aina chache za aina za cyakula kutoka nje ya nchi ikiwemo mchele,sukari na unga wa ngano ambapo kwa mwaka 2020 uzalishaji wa ndani wa mazao ya chakula ulikuwa ni wa kujitosheleza kwa zaidi ya asilimia sabiini (70%).

 

Kwa mwaka 2020 uzalishaji wa muhogo ulikuwa ni tani laki moja,elfu hamsini na nane,mianne na sitini na tano (158,465/=)Uzalilishaji wa mpunga ulikuwa ni tani elfu arobaini,mia tatu na ishirini na nane(40,328) na ndizi tani elfu sitini na tano,mia tatu na ishirini na moja.(65,321).

 

Akizungumzia takwimu za magonjwa Mhe. Hemed alisema Zanzibar ina asilimia saba nukta tano (7.5%) ya wagonjwa wa kisukari na asilimia thelasini na tatu wagonjwa wanakabiliwa na tatizo la shindikizo la juu la damu, ingawaje uwepo wa chakula cha kutosha haumsaidi mtu kupata lishe sahihikutokana na kukosekana kwa umakini wa matumizi mazuri ya ulaji wa chakula.

 

“Hali hii inaonesha kuwa, kuna haja ya kuweka mikakati imara ya kuimarisha masuala ya lishe kwa wananchi wote hata wale wenye chakula cha kutosha” Alisisitiza Mhe. Hemed

 

Katika kuipatia ufumbuzi changamaoto hiyo Makamu wa Pili wa Rais alilipongeza shirika la chakula duniani (FAO) kwa kushirikiana na wadau wengine kwa kuandaa mkakati wa muongozo wa ulaji wa chakula wa muda mfupi ujao.

 

Wakati nchi ikielekea katika msimu wa mvua za vuli Mhe. Hemed aliwataka wakulima, wafugaji Pamoja na wavuvi kufuatilia na kuzingatia ushauri unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Tanzania (TMA) hasa kwa wakulima kupanda mazao yanayoendana na mvua hizo ili kuepuka hasara na ukosefu wa chakula unaoweza kutokea Zanzibar.

 

Makamu wa Pili wa Rais alieleza kwamba, kwa vile Zanzibar imezungukwa na bahari kuna ulazima kwa watu wake kuongeza uzalishaji wa Samaki na mazao mengine ya baharini ili kuimarisha lishe za wananchi kwa kuzingatia uvuvi endelevu unaolinda mazingira ya bahari yakiwemo matumbawe na fukwe.

 

Akisoma risala katibu Mkuu wizara ya Kilimo umwagiliaji, maliasili na mifugo Ndugu Maryam Juma Sadala alieleza wizara imeamua kufanya maaadhimisho hayo kwa kufanya kongamano lengo likiwa ni kupata maoni kutoka kwa wadau kwa ajili ya kuimarisha Afya za wananchi.

 

Katibu Maryam alisema Wizara ya  kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itaendelea kutoa elimu kwa wananchi inayohusiana na masuala ya chakula bora ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kuwapatia lishe bora wananchi wake.

 

Akizungumzia kuhusu suala la UVIKO-19 Katibu huyo alibainisha kuwa, maradhi hayo yameisababishia dunia kukumbwa na janga la njaa ambapo takwimu zinaonesha idadi ya watu wanaokubwa na balaa la njaa limeongezeka kutoka watu Millioni Sita hadi Millioni Mia Nane Duniani kote.

 

Akigusia changamoto zinazoikabili wizara hiyo katibu Maryam alisema uchache wa watalamu na kukosekana kwa nyenzo za usarifu wa mazao baada ya kilimo jambo linapelekea upotevu wa mazao baada ya mavuno.

 

Nae, Mwakilishi mkaazi wa umoja wa Mataifa Dorothy Temu Usiri alieleza takribani watu Billioni tatu duniani wanashindwa kumudu chakula chenye Afya, hivyo ameishauri jamii kuimarisha mifumo ya chakula kwani kufanya hivyo kutasaidia kutoa tija ikiwemo kuizleta Pamoja familia.

 

Maadhimisho ya siku ya chakula duniani hufanyika kila kila ifikapo Oktoba  16, ambapo kauli mbiu yam waka huu inasema “ ZINGATIA UZALISHAJI NA MAZINGIRA ENDELEVU KWA LISHE NA MAISHA BORA”.

 

Mapema Makamu wa Pili wa Rais alipata fursa ya kutembelea maonesho ya wakulima na kuskiliza mafanikio na changamoto zao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.