Habari za Punde

Waziri Mhe.Mwambe; Rais Samia amedhamiria kumilikisha Wananchi Uchumi

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe akipata maelezo ya shughuli za uwekezaji  kutoka kwa mtaalamu wa madini, wa mgodi wa Bulyanhulu, Damir Zloic.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe (Katikati), akiwa kwenye vazi maaluum kwa ajili ya kukagua shughuli za uwekezaji katika mgodi wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga, kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kahama , Festo Kiswaga na kulia kwake ni Mbunge wa jimbo la Msalala Idd Kasimu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe akiwa kwenye vazi maaluum kwa ajili ya kukagua shughuli za uwekezaji katika mgodi wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga, ambapo ameambatana na wataalamu wa ofisi yake,  pamoja na wa mgodi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe (watatu kulia) akiwa kwenye vazi maaluum kwa ajili ya kukagua shughuli za uwekezaji katika mgodi wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga, ambapo ameambatana na wataalamu wa ofisi yake, pamoja na wa mgodi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe akiangallia mashine ya inayotumiaka katika utengenezaji wa samani na kikundi cha wilayani Kahama            

Na.Ibrahim Hamidu.                                                                                                                                     
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe ameeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kumilikisha wananchi uchumi, kupitia  vituo vya  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambavyo kwa sasa vipo katika mikoa 17 chini ya uratibu wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.                          

Akiongea mara baada ya kukamilisha ziara yake katika Manispaa ya Kahama. Mhe. Mwambe amefafanua kuwa Mhe. Rais Samia anatekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 na muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2020-2025.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mwambe amezitaka halmashauri nchini ambazo bado hazijaanzisha vituo hivyo kama cha Kahama. Kituo hicho hadi kufikia mwezi Novemba 2021, zaidi ya wananchi 19,120 wamehudumiwa na jumla ya mikopo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 46.86 imetolewa hadi kufika Septemba 2021 kwa waombaji walio katika sekta mbalimbali kama vile, kilimo; mifugo; biashara; na uvuvi.

Aidha, Mhe Mwambe   ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuandaa na kutenga maeneo ya uwekezaji ikiwemo eneo la viwanda la Ummy Mwalimu ambalo limegawiwa kwa wawekezaji wa Biashara na Viwanda vidogo ambapo hadi sasa ajira 2,754 zimezalishwa katika eneo hilo.

Akiwa katika ukaguzi wa shughuli za Uwekezaji na Maendeleo ya Sekta Binafsi wilayani humo katika eneo la Uwekezaji la Chapulwa kwenye Kiwanda cha Kampuni ya KOM Foods Products, Mhe. Mwambe alielezwa na Mwekezaji huyo changamoto ya umeme wa megawati 9 ndio unaochelewesha uzalishaji wa vinywaji na usindikaji wa vyakula katika viwanda nane vinavyojengwa na mwekezaji huyo.

Mhe. Mwambe alimhakikishia Mwekezaji huyo kushirikiana na Wizara nyingine za kisekta katika kutatua changamoto hizo ili uwekezaji huo uweze kuzalisha ajira, kuongeza mapato nchini.

Aidha, Mhe. Mwambe alitembelea na kufanya mazungumzo na viongozi wa mgodi wa Bulyanhulu ambapo aliwapongeza wawekezaji hao kwa kuongeza ajira nchini kwa kuajiri watanzania wengi wakiwamo watu ambao wanaowazunguka pamoja na kuwapatia nafasi za usambazaji wa didhaa mgodini hapo.

Aidha, Mhe. Mwambe aliwakumbusha wawekezaji hao kutekeleza makubaliano ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami  kutoka Bulyanhulu  hadi Kahama yenye Urefu wa Kliometa 75. Kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea shughuli za uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Ziara hiyo ya siku moja katika Manispaa ya Kahama inalengakutembelea na kukagua miradi ya Uwekezaji, shughuli za uwezeshaji  wananchi Kiuchumi, vile vile kufanya mikutano ya mashauriano na kujadili changamoto  na Mhe, Waziri Mwambe kupendekeza namna bora ya  kuzitatua.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.