Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Awaongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Marehemu Al Noor Kassum

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Salim Kassum ambaye ni Mtoto wa marehemu  Al noor Kassum (wa pili kulia) na Muwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Agha Khan nchini Tanzania Amin Kurji wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyekua Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya  pili,  Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Novemba 20, 2021
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki  katika dua wakati alipoongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na  Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili,  Al noor Kassum, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na  Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya  pili, Mzee Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam 
Waziri Mkuu Mstaafu David Cleopa Msuya akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Mzee Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na  Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya pili, Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyekua Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti wa serikali ya  awamu ya kwanza na ya  pili,  Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuwaongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekua Waziri wa Fedha na Utawala wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na aliyekua Waziri Mstaafu wa Wizara tofauti kwenye serikali ya awamu ya kwanza na ya  pili,  Al noor Kassum, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 20, 2021.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.