Habari za Punde

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan Jana Ameongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Jijini Dodoma.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kabla ya kuaza kwa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi kilichotanguliwa na Semina ya Sensa ya Watu na Makaazi Tanzania
WAJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma,wakishiriki katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichotanguliwa na Semina ya Sensa ya Watu na Maakazi Tanzania, wa kwanza Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakiwa wamesimama wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa amae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika ukumbi
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma na (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Ali Mohamed Shein na (kushoto kwake) Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg. Daniel Chongolo, wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, wakati wa hafla ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi kilichotanguliwa na Semina ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makaazi Tanzania
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiongoza na Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma na kutanguliwa na Semina ya Sensa ya Watu na Makaazi Tanzania.
WAJUMBE wa Kikao cha Halmashari Kuu ya Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mhe.Samia Suluhu Hassan.(hayupo pichani) akiongoza Kikao hicho cha kawaida kilichotanguliwa na Semina ya Sensa ya Watu na Makaazi Tanzania 2022
KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makaazi Tanzania Mhe.Anna Makinda akizungumza wakati wa Semina ya Sensa na Makaazi Tanzania iliowashirikisha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo 18-12-2021
MTAKIMWI Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa akiwasilisha Mada ya zoezi la Sensa ya Watu na Makaazi Tanzania 2022, wakati wa Semina hiyo kwa Wajumbe wa Kikao cha Halmashairi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, iliyofanyika kabla ya kuaza kwa Kikao cha kawaida cya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
WAJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma,wakishiriki katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichotanguliwa na Semina ya Sensa ya Watu na Maakazi Tanzania, wa kwanza Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakiwa wamesimama wakati Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa amae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, akiwasili katika ukumbi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.