Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameongoza Wananchi katika Sala ya Kuusalia Mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa Aliyewahi Kuu Mbunge wa Mpendae Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, iliofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu Sheikh Mahmoud Mussa Ngwali , baada ya kumalizika kwa sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa,(Baharia) Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
BAADHI ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wakiitikia dua ikisomwa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Ngwali baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
WANANCHI wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) baada ya kumalizika kwa Sala na dua ya kumuombea marehemu iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Iria Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
WANANCHI wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) baada ya kumalizika kwa Sala na dua ya kumuombea marehemu iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kijiji cha Iria Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Issa Kassim Issa (Baharia) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar, baada ya kuwekwa mwili wa marehemu, maziko yaliyofanyika katika makaburi ya familia katika Kijiji cha Pongwe Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Kombo Hassan Ali, baada ya kumalizika kwa maziko ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja Marehemu Issa Kassim Issa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar.maziko hayo yamefanyika katika makaburi ya familia Kijiji cha Pongwe Wilaya ya Kati Unguja.
WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakiitikia dua ikisomwa na Sheikh Twaha Hassan Ali (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa maziko wa Marehemu Issa Kassim Issa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Sheikh Abdulazazi Saleh Juma,(hayupo pichani) alipofika nyumba kwa marehemu katika Kijiji cha Uroa kutowa mkono wa pole kwa familia.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa na Vizuka wa Marehemu Issa Kassim Issa, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mpendae Zanzibar,wakiitikia dua ikisomwa na Sheikh.Abdulazizi Saleh Juma,(hayupo pichani) baada ya kutowa mkono wa pole kwa Familia ya alipofika nyumbani kwa marehemu Kijiji cha Uroa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.