AFISA utawala wa Hoteli ya
The Manter Resort Zamda Hussein (katikati), akitoa maelezo juu ya mifumo ya
usajili wa wageni na utoaji wa risiti za kielektroniki kwa wateja baada ya kupata
huduma katika hoteli hiyo, kwa wajumbe wa kamati ya Uchumi ya Baraza la
Wawakilishi Zanzibar, kulia mwenyekiti wa kamati hiyo Sabiha Filfil Thani na
kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim
Ali.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
AFISA utawala wa Hoteli ya
The Manter Resort Zamda Hussein, akionyesha mashine ya utoaji wa Risiti za
Kieletronik (VFMS)jinsi zinavyofanya kazi katika uingizaji wa taarifa za
wageni, kwa wajumbe wa kamati ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar,
kulia mwenyekiti wa kamati hiyo Sabiha Filfil Thani na kushoto ni Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MWENYEKITI wa kamati ya
Uchumi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Sabiha Filfil Thani, akiangalia jinsi
mashine ya utoaji wa risiti za Kieletronik (VFMS) inavyofanya kazi, kushoto ni
Afisa utawala wa Hoteli ya The Manter Resort Zamda Hussein, wakati wajumbe wa
kamati ya Uchimi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilipotembelea hoteli hiyo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
KAMISHNA wa Bodi ya Mapato
Zanzibar (ZRB) Salum Yussuf Ali, akitoa ufafanuzi wa maswali ya wajumbe wa Kamati
ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, walipotembelea hoteli na kukagua
mifumo ya utoaji wa Risiti za kielektroniki.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MKURUGENZI wa Mifumo ya
kimtandao kutoka ZRB (IT) Harith Abdilazizi Ahmada, akitoa ufafanuzi kwa
wajumbe wa kamati ya Uchumi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, juu ya ufanyaja
kazi wa mashine za utoaji wa risiti za kielektronik zinavyofanya kazi na ZRB
wanavyoona kila kinachofanyika.(PICHA NA
ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MWENYEKITI wa Kamti ya
Uchumi ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Sabiha Filfil Thani(kulia), akifuatiwa
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali,
wajumbe wa kamati ya uchumi Nadir Abdullatif Yussuf na Ameir Abdalla Ameir, wakisikiliza
maelezo kutoka kwa meneja Mkuu wa Hoteli ya The Aiyan.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment