Na Raya Hamad - OMKR
Imeelezwa kuwa sheria
mpya ya Watu wenye Ulemavu inayokuja itahakikisha kuna kipengele kinacholazimisha
kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mtu yeyote atakaemficha mtoto au mtu mwenye
ulemavu
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Dkt Saada Mkuya Salum ameyasema hayo wakati
akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kwa
kipindi cha Octoba hadi Disemba 2021, mbele ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi
inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa katika Ukumbi mdogo wa mkutano
Gombani.
Dkt Saada amesema
Baraza la Taifa la Watu wenye Ulemavu katika kuyatafutia ufumbuzi changamoto za
Watu wenye Ulemavu limefanya ziara mbali mbali kusikiliza changamoto, vikwazo na
malalamiko ya walengwa kwa lengo la kuyapatia ufumbuzi likiwemo baadhi ya
wanajamii kuwaficha watoto wenye ulemavu na kuwakosesha haki zao za msingi
Aidha Ofisi yake
imeanza kutoa mafunzo ya lugha ya alama kwa watendaji wa Serikali kutoka
taasisi 17 kwa ajili ya kuwapatia taaluma ili Watu wenye Ulemavu wa Uziwi
waweze kuhudumiwa bila kipingamizi wanapohitaji huduma kutoka kwenye taasisi
zote za Serikali na binafsi
Akizungumzia kuhusu
suala la miradi iliyofanyiwa tathmini za athari za kimazingira Dkt Saada
amesema baada ya kufanyika tathmini hio kwa miradi ya maendeleo ya kiuchumi
hutolewa vyeti vya mazingira na masharti yay a kimazingira ambayo husaidia
kupunguza uharibifu na uchauzi wa mazingira na kuifanya miradi kuwa endelevu
Pia Mamlaka ya Usimamizi
wa Mazingira ZEMA imefanya ziara ya kufatilia mazingira kwa miradi saba 7 ya
kiuchumi na matokeo ya ziara hizo ni kuongezeka kwa mwamko wa wawekezaji katka
kudhibiti athari za kimazingira kwenye miradi yao
“mambo makubwa
yaliyobainika kwenye ziara hizo tumeona Hoteli nyimgi zimeanza kuzingatia
masuala ya kimazingira ikiwa ni pamoja na kutenganisha taka za kuoza na
zisizooza, kuimarisha maeneo ya kimazingira na kudhibiti maji machafu”
alilisistiza Dkt Saada
Kuhusu Dawa za Kulevya
Dkt Saada amesema Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais inashirikiana na Mamlaka
mbalimbali za Serikali katka mapambano dhidi ya Dawaza Kulevya zikiwemo Jeshi
la Polisi, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali
na Mahakama hususan katka masuala mbalimbali yanayohusiana na udhibiti na
uchunguzi wa kesi za Dawa za Kulevya.
Dkt Saada pia
ameiyambia Kamati hio kuwa Tume ya UKIMWI ambayo ina jukumu la uratibu,
ufatiliaji na tathmini juu ya muitiko wa Taifa wa UKIMWI na mawasiliano na utetezi
wa masuala ya VVU na UKIMWI katika kipindi cha Octoba hadi Disemba 2021 pamoja
na mambo mengine imeratibu na kusimamia kampeni za kijana kataa UKIMWI
Kufanya ziara za ufatiliaji
na tathmini kwa vituo vinavyotoa huduma za UKIMWI (CTC) vya Hospitali ya
Abdalla Mzee, Chake Chake, Micheweni na Wete pamoja na vituo vya huduma rafiki
Mkoani, Mbuzini, Bwagamoyo na ZAYEDESA Mkoani Pemba
Aidha Tume ya UKIMWI
imefanya mikutano uliwashirikisha wadau 25 kwa lengo la kutoa maoni juu ya
maandalizi ya mpangp Mkakati wa Mapambano dhidi ya UKIMWI, jumla ya taasisi 12
zilitembelewa kwa lengo la kukusanya maoni juu ya maandalizi ya mkakati huo wa
5 wa UKIMWI
Akielezea changamoto
Dkt Saada amesema kumekuwa na ongezeko kwa tabia hatarishi kwa vijana na jamii
hata hivyo kampeni mbali mbali za elimi ya kinga kuhusu UKIMWI inaendelea
kutolewa kwa ujumla pamoja na ushauri nasaha na upimaji wa hiari wa VVU
Upungufu wa baadhi ya
watumishi wa Idara na Taasisi za Pemba ikiwemo Ofisi ya Faragha ambapo kwa sasa
wameazima kutoka taasisi nyengine, kukosekana kwa jengo la Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Pemba ambapo tayari jitihada zinaendelea za kutafuata jengo kwa
ajili ya Ofisi Kuu
Nae mwenyekiti wa
Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa
Mhe Hassan Hafidh ameiomba Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuharakisha
kuzifanyia marekebisho sheria zote zilizobakia ikiwemo ile ya UKIMWI na Watu
wenye Ulemavu na Mazingira ili mabadiliko ya kiuchumi yaendane na sheria za
nchi kwa maslahi ya Taifa na wananchi
Mhe Hassan pia ameishauri Ofisi ya Mkamu wa Kwanza wa Rais pamoja na kuviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha magari yanayowachukuwa viongozi wa Kitaifa wakati wakiwa kwenye misafara yawe mazima na yawe yanamilikiwa na Serikali sio binafsi ama taasisi binafsi kwa maslahi ya nchi
No comments:
Post a Comment