Habari za Punde

Hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofaulu Mchipuo na Vipawa maalumu kutoka skuli nne za Pemba

MRATIB wa Taasisi ya Milele Zanzibar Foundation Pemba Abdalla Said Abdalla, akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofaulu Mchipuo na Vipawa maalumu kutoka skuli nne, ambazo zimefanya vizuri kutoka katika shehia zinazonufaika na miradi ya Milele, hafla iliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

MKUU wa Miradi kutoka Taasisi ya Milele Zanzibar Khadija Ahmed Shariff, akizungumzia mikakati ya Milele Zanzibar katika kusaidia jamii, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi 64 waliofaulu mchipuo na vipawa, kutoka katika skuli zilizofanya vizuri ambazo zinanufaika na miradi ya Milele hafala iliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

KAIMU Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, pia ni Afisa ELimu Sekondari Pemba Suleiman Hamad Omar, akizungumza na wanafunzi, walimu katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi 64 waliofaulu mchipuo na vipawa, kutoka skuli zilizofanya vizuri ambazo zinanufaika na miradi ya Milele hafala iliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)

KAIMU Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, pia ni Afisa ELimu Sekondari Pemba Suleiman Hamad Omar, akimkabidhi Mkoba, mabuku na kampasi mwanafunzi Yassir Khator Nassan kutoka Mnarani Makangale, ambaye amefanikiwa kupasi vipawa maalumu, hafla iliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA

BAADHI ya wanafunzi waliofaulu na kupasi michipuo na Vipawa , kutoka skuli ambazo zinanufaika na miradi ya Milele zanzibar, wakiwa na mikoba hiyo baada ya kukabidhia na taasisi hiyo hafla iliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA

BAADHI ya wanafunzi waliofaulu na kupasi michipuo na Vipawa , kutoka skuli ambazo zinanufaika na miradi ya Milele zanzibar, wakiwa na mikoba hiyo baada ya kukabidhia na taasisi hiyo hafla iliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA


 KAIMU Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, pia ni Afisa ELimu Sekondari Pemba Suleiman Hamad Omar, akimkabidhi shilingi laki nane(800,000/=)Mwalimu Ali Massoud Ali, kufuatia skuli yake ya Mnarani Makangale kupasisha wanafunzi zaidi ya 20 mchipuo na vipawa katika mitihani iliyopita, hafla iliofanyika mjini Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.