Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Ikulu.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake (kulia kwa Rais) Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe.Didier Chassot, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza na kuzungumza na mgeni wake Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot,alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Mlango wa Zanzibar (Zanzibar Door) mgeni wake Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe.Didier Chassot, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na mgeni wake Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe.Didier Chassot, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na kuzungumza na mgeni wake Balozi wa Switzerland Nchini Tanzania Mhe.Didier Chassot, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu) 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepongeza utayari wa Serikali ya Switzerland kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika jitihada zake za maendeleo.

Rais Dk. Mwinyi pia, alipata fursa ya kuzungumza na Balozi wa Switzerland nchini Tanzania Didier Chassot na kumpongeza kutokana na kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika nyanja mbali mbali ikiwa ni pamoja na kusaidia sekta ya afya, kuanzisha Bima ya Afya, utawala Bora, kuijengea uwezo Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi (ZAECA), Ofisi ya Mkuu wa Mashtaka pamoja na kuzisaidia Asasi za Kiraia (NGOs) za hapa nchini.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Serikali ya Switzerland kwa kusaidia juhudi za Serikali za kuanzisha Bima ya Afya hapa Zanzibar ambapo matarajio makubwa kwamba katika mwaka ujao wa fedha Bima hiyo itaanza sambamba na kusaidia vifaa katika kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19.

Nae Balozi wa Swiitzerland Didier Chassot alitoa ahadi kwa Rais Dk. Mwinyi kwamba Serikali yake itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika nyanja mbali mbali ikiwemo afya pamoja na Utawala Bora.

Katika maelezo yake Balozi huyo wa Switzeland alimueleza Rais Dk. Mwinyi hatua zinazochukuliwa na nchi yake katika kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea katika kuisaidia Zanzibar.

Balozi Didier Chassot alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa juhudi zake za kuwa karibu na Asasi za Kiraia pamoja na juhudi zinazochukuliwa na Serikali anayoiongoza katika kuziwekea mazingira mazuri Asasi hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.