Habari za Punde

TRA TANGA WAIKABIDHI WILAYA YA BUHIGWE PIKIPIKI MBILI KWA AJILI YA KUWASAIDIA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA KITAIFA

KAIMU Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga  Davis Mongate kushoto akimkabidhi pilikipiki mbili Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Kanali Michael Ngayalina kwa ajili ya kuwasaidia kutekeleza majukumu ya Kitaifa leo Jijini Tanga

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga leo wameikabidhi wilaya ya Buhigwe ya Mkoani Kigoma pikipiki mbili kwa ajili ya kuwasaidia katika majukumu mengine ya kitaifa

Pikipiki hizo zilikamatwa na maofisa wa TRA kwa nyakati tofauti wakati wakifanya doria ambazo zilikutwa zikiwa vimebeba biashara ya magendo huku watuhumiwa wakikimbia

Halfa ya makabidhiano hayo imefanyika leo mkoani Tanga ambapo Kwa niaba ya Meneja wa Mkoa wa Tanga Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga na Kamishna wa Forodha, Davis Mongate .

Alisema leo ni siku ramsi ya kuzikabidhi kwa Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Kanali Michael Ngayalina ili ziweze kuwasaidia majukumu mengine ya kitaifa ambazo zilikamatwa wilaya Pangani zikiwa zimepakia madumu ya mafuta ya magendo.

Aidha alisema maafisa hao walizikamata na wahusika walikimbia na kuzitekeleza pikipiki hizo na Kamisha wa forodha alizigawa kwa Mkuu wa wilaya ya Buhigwe ambapo huo ni utaratibu wa mamlaka vitu ambavyo vinakamatwa kinyume cha utaratibu zinagawiwa kwenye taasisi za serikali .

Akizungumza mara baada ya kupokea pikipiki hizo, Kanali Michael alimshukuru Kamisha wa Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA Tanzania na Wizara ya Fedha kwa niaba ya wananchi wake kwa kuwapatia vyombo hivyo vya usafiri ambazo zilikamatwa zikifanya shughuli za magendo.

Alisema wilaya yao bado inachangmoto nyingi za kiusalama lakini kibiashara ni wilaya ya mpakani hivyo pikipiki hizo zitawasaidia shughuli za doria na biashara mpakani na biashara inayokinzana na sheria, kanuni za serikali hususani idara ya mapato pikipiki hizo zitawasaidia.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi ni vizuri wakafuata sheria ,taratibu na kanuni kwenye ufanyaji biashara kwani wizara ya fedha imeeleza wananachi kutoa kodi mbalimbali na kufuata utaratibu uliotolewa na serikali kufanya biashara na kuepuka na vitendo vinavyokinzana na sheria hususani magendo.

“Hapa nimeambiwa wamiliki wa pikipiki hizi walikimbia baada ya kukamatwa na maafisa wa idara ya forodha tunaomba wananchi fuateni sheria na kanuni tufanye biashara na kupekna na kukidhana na vyombo hivyo “Alisema

“Tumekuja kuvifuata baada ya kupokea taarifa kwamba tumegawiwa hivyo tutakwenda kuvitumia kwa shughuli za kibiashara na kiusalama kwani wilaya ina takribani kilomita 60 za mpaka na Burundi na changamoto za kiusalama na biashara ni kubwa tunahaidi vyombo hivi vitatumika kwa shughuli hizo na sio nyenginevyo”Alisema

Awali akizungumza kwa niaba ya Meneja wa Mkoa wa Tanga Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga na Kamishna wa Forodha, Davis Mongate alisema leo wamemua kuzigawa pikipiki kwa Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma kwa ajili ya kusaidia majukumu ya Kitaifa ambapo zilikamatwa wilaya ya Pangani zikiwa zimepakia madumu ya mafuta na wenye pikipiki walikimbia.

Alisema huo ni utaratibu wa mamlaka kwamba vitu ambavyo vinakamatwa kinyume na taratibu vinagawiwa kwa Taasisi za Serikali zenye upungufu wa vyombo vya usafiri kwa hizo pilipiki zitakabidhiwa kwa mkuu wa wilaya ya Buhigwe .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.