Habari za Punde

WAZIRI WA AFYA AZUNGUMZA NA UJUMBE KUTOKA ALMA

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akifanya  mazungumzo na Shirika la Viongozi wa Afrika (ALMA ) yenye lengo la kuimarisha  Sekta ya Afya katika maradhi mbalimbali yakiwemo malaria na maradhi yasiyoambukiza,huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Unguja walipofika kujitambulisha.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Dkt. Fatma Mrisho (kulia) akimkabidhi zawadi maalum Mwenyekiti wa Shirika la Viongozi wa Afrika (ALMA ) Joy Phumaphi alipofika katika Ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar na Ujumbe wake kujitambulisha.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii,Wazee,Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akimpatia maelekezo Mwenyekiti wa Shirika la Viongozi wa Afrika (ALMA ) Joy Phumaphi kuhusu karafuu inayopatikana Zanzibar mara alipofika katika Ofisi za Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar na Ujumbe wake kujitambulisha.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

Na.Sabiha Khamis -- Maelezo Zanzibar.                     

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto imesema wizara ipo tayari kushirikiana na Shirika la Viongozi wa Afrika katika mambo mbali mbali ikwemo kuimarisha sekta ya Afya.

Akizungumza na ujumbe kutoka Shirika hilo huko ofisini kwake Mnazi mmoja, Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui amesema amefurahishwa na ujio wa ujmbe  huo na kuahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha sekta ya Afya inazidi kuimarika nchini.

Amesema ujumbe huo una lengo la kuisaidia sekta hiyo katika mambo mbali mabli ya kiafya ikiwemo kutokomeza kabisa maradhi ya malaria katika jamii.

“Ingawa malaria yamepungua kwa kiasi kikubwa nchini na kufikia asilimia moja lakini  ipo haja ya kupunguza maradhi hayo na kuyaondosha kabisa” amesema Waziri.

Aidha amefahamisha kuwa shirika hilo linampango wa kusaidia na kupambanana  maradhi yasioambukiza kama vile sindikizo la damu, kisukari, saratani, kichocho na mengine mengi ambayo hayaambukizi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika hilo Joy Phumaphi Shirika hilo lipo tayari kuhamia Zanzibar na kufanyakazi na Wizara ya Afya katika kuhifadhi afya za wananachi wa Zanzibar.  

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ameahidi kutoa ushirikiano na Wizara ya Afya ya Zanzibar katika kuimarisha afya kwa wananchi na kupunguza vifo kwa wanawake na watoto.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.