Habari za Punde

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Amemuwakilisha Rais wa Tanzania Mhe.Samia Katika Ufunguzi wa Mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama Afrika - 2

 








Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo, kuingia kwenye ukumbi wa TANAPA jijini Arusha kwa ajili ya  ufunguzi wa mkutano  wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika,  Februari 28, 2022.  Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo (wa nne kushoto) na Rais wa Mahakama ya Afrika, Imani Aboud ( wa tano kushoto) wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Wa pili kulia ni Waziri wa katiba na Sheria, George Simabachawene na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella. Wengine pichani ni Majaji wa Mahakama hiyo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Mahakama hiyo Imani Aboud, alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea nembo ya Mahakama ya Afrika kutoka kwa Rais wa Mahakama hiyo Imani Aboud, alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo. 

Baadhi ya washiriki wa ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa mkutano wa 64 wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika, Jijini Arusha, Februari 28, 2022. Mgeni rasmi katika ufunguzi huo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Shirikisho (Majimbo) ya Nigeria Prof. Yemi Osibanjo.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.