Habari za Punde

Mshindi wa Tuzo ya Fasihi Prof Abdulrazak Gurnah Apokelewa kwa Aina yake kwa Ngoa za Asili ya Utamaduni wa Zanzibar.

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akizwa na mgeni wake Prof.Abdulrazak Gurnah mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi,alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said mchana wa leo amempokea mshindi wa tuzo ya Nobel ya Fasihi(2021) Profesa Abdulrazak Gurnah katika Kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume.

Prof Gurnah ambae pia ni mshindi tuzo ya waandishi wa Jumuiya ya Madola(Commonwealth Writers Prize 2006) yuko Zanzibar kwa ajili ya Tamasha Utamaduni na Utalii Afrika( FESTAC AFRICA) linalotarajiwa kuanza kesho na  kufunguliwa  rasmi  na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika hoteli ya Hotel Verde.

Aidha, Prof Gurnah ambae ni mzaliwa wa Zanzibar atapata pia nafasi ya kutembelea baadhi ya skuli ikiwemo skuli ya Lumumba ambayo ndio aliyosoma akiwa mtoto.


Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi(2021) Profesa Abdulrazak Gurnah akimtunza msanii mkongwe wa Sanaa ya Taarab Zanzibar Profesa Mohammed Ellys, wakati wa mapokezi yake alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi(2021) Profesa Abdulrazak Gurnah akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar.(hawapo pichani) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.