Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiteremka ndege ya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi pamoja na Maafisa mbali mbali akitokea katika nchi ya Burundi kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya nchi hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akitokea Nchi ya Burundi kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan katika sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya nchi hiyo.
Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amerejea nchini leo akitokea
Burundi ambapo alihudhuria sherehe za miaka 60 ya Uhuru wa nchi hiyo.
Katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi alipokewa
na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed
Suleiman Abdullah.
Rais Dk.
Mwinyi ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, katika safari yake hiyo alifuatana na viongozi mbali mbali wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar akiwemo mkewe Mama Mariam Mwinyi.
Imetayarishwa na Idara ya
Mawasiliano,
Ikulu Zanzibar.
No comments:
Post a Comment