Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI MIKUMI MOROGORO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa pamoja na viongozi mbalimbali wakati alipowasili Hifadhi ya Taifa ya Mikumi mkoani Morogroro leo tarehe 16 Agosti 2022. Hapo kesho tarehe 17 Agosti 2022 Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Magari maalum yatakayotumika katika kuboresha Miundombinu ya Utalii yaliotolewa na Mradi wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW) Mikumi mkoani Morogoro.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.