Habari za Punde

MUSWADA WA SHERIA YA USIAMAMIZI WA MAAFA WAWASILISHWA KWA KAMATI.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati ofisi hiyo ikiwasilisha   Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa kilichofanyika Agosti 30, 2022 Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imewasilisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.

Kikao hicho kilihusisha viongozi mbalimbali  kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene, na Naibu Waziri wake  Mhe. Ummy Nderiananga. Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu pamoja na  Naibu wake Bwa. Kaspar Mmuya.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga akiwasilisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Agosti 30, 2022 Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akieleza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Bunge

Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Yahaya Masare  (katikati) akichangia hoja wakati wa kikao hicho.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.