Habari za Punde

Ushauri wa CCM Kwa Wizara ya Kilimo Kujenga Kiwandsa cha Kuchakata Tumbaku.

Katibu wa nec ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfuluma, Wilaya ya Uyui mkoani Tabora akiwa katika ziara ya kukagua Uhai wa chama na Utekelezaji wa Ilani ya I chaguzi ya CCM ya 2020-2025.P
icha zote na Fahad Siraji wa CCM).

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimeshauri na kupendekeza kwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kujenga kiwanda cha kuchakata tumbaku pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza sigara ndani ya Mkoa wa Tabora kwani kuna kila sababu ya kuwa na viwanda hivyo kutokana na mkoa huo kuwa kinara wa zao hilo nchini.

Amefafanua Tabora imeongoza uzalishaji tumbaku kutoka kilo milioni 16 mpaka kilo milioni 33 rai ya CCM kwa Wizara ya Kilimo umefika wakati wa kuangalia haraka iwezekanavyo kujenga kiwanda cha kuchakata tumbaku mkoani Tabora kwani ndiko kilimo hicho kimepamba moto. Aidha alitumia nafasi hiyo kuwashauri wakulima wa tumbaku wasikubali kupangiwa ekari za kulima , bali kila mkulima aachwe alime kulingana na uwezo wake. Ameongeza CCM CCM inafuatilia kwa karibu kwani waliahidi kwenye Ilani ya Uchaguzi na sasa wana kazi ya kufuatilia yale waliyokubaliana yanatekelezwa huku akiwahakikisha na yeyote mwenye nia au dhamira ya kuhujumu jitihada hizo hawatamzama machoni.
“Tuliahidi na leo tunatekeleza , nataka niwaambie siri moja ya CCM kuendelea kubaki madarakani ni namna ambavyo tunaahidi na kutekeleza mbele ya watanzani na hiyo sifa tutaiendeleza kwasababu tunaye kinara, jemedari , mpiganaji lakini tunaye mtu aliyeamua kuyabeba maono yenu ambaye ni Rais Samia na kwa kuwa tunaye jemedari wetu CCM itaendelea kutawala miaka 100 ijayo,”alisema.

Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Mheshimiwa Almasi Maige amezungumzia Umuhimu wa Ujenzi wa Kiwanda Cha Tumbaku kujengwa katika Wilaya Hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.