Habari za Punde

Wajumbe wa BLW Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ziarani Butiama

Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa wakiwa nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama Musoma wakiwa wameambatana na maafisa mbali mbali kutoka TASAF Bara na Zanzibar kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Mwitongo wilayani Butiama ikiwa ni sehemu moja ya kujifunza namna bora ya kuwaenzi Viongozi wakuu.
Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa Mhe Machano Othman Said akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama. Wengine wanaoonekana na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo pamoja na maafisa wengine kutoka Tasaf Bara na Zanzibar.

 Muongoza wageni wa maeneo ya historia nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwitongo Butiama Bi. Gaudensia Waziri akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu kuhusu Kaburi na historia ya Chifu Burito aliyekuwa chifu wa Kabila la Wazanaki

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.