Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Amekutana na Kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA Bw.Ali Abdalla Ali alipofika Ofosini kwake Migombani Unguja Jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, leo tarehe 21 Septemba, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA), Bw. Ali Abdallah Ali.

Mkurugenzi Ali amefika Ofisini kwa Makamu Migombani Mjini Zanzibar, kwalengo la kujitambulisha na kubadilishana mawazo katika mambo mbali mbali.

Kitengo cha Habari

Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar

Septemba 21, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.