Habari za Punde

Serikali itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kuhusiana na uimarishaji wa sekta ya Afya  walipofika Ofsini  kwake Mnazimmoja Kujitambulisha.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
Mshauri Mkuu wa Shirika la Misaada  la Marekani  (USAID)Mrgaret Taylor akizungumza na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui kuhusiana na mambo mbalimbali ya kuimarisha  Sekta ya  Afya  wakati alipofika na ujumbe wake  Kujitambulisha huko Wizara ya Afya Mnazimmoja Zanzibar.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi zawadi maalum Mshauri Mkuu wa Shirika la Misaada  la Marekani (USAID )Mrgaret Taylor mara baada ya kufika ofisini kwake na Ujumbe wake Kujitambulisha .PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.

 Na Rahma Khamis Maelezo –Zanzibar                   20/9/2022

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la USAID ili kuweza kuimarisha sekta ya  afya hapa nchini.

Amesema Shirika la USAID limekuwa likisaidia Sekta ya Afya katika Nyanja tofauti ikiwemo Malaria, Kifuakikuu, homa ya Ini na huduma nyengine za kijamii.

Akizungumza na Mshauri Mkuu wa Shirika la USAID Magret Toylor huko ofisini kwake Mnazimmoja  Waziri Mazrui amesema  kutokana na jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Washirika wa Maendeleo mbali mbali wakiwemo USAID Wizara ya Afya imeweza kupiga hatua katika kupambana na Malaria ambapo kwa sasa yapo chini ya asilimia moja.

Amefahamisha kuwa USAID imeweza kusaidia katika kudhibiti ugonjwa wa ukimwi ambayo yameathiri sana ambayo yanaathiri sana nguvu kazi ya watanzania ambapo kwa sasa UKIMWI hapa Zanzibar umepungua kwa kiasi kikubwa wamefikia malengo ya 90, 90, 90 na Wizara inafanya jitihada ya kufikia malengo ya 95, 95 na watoto wachanga wanaozaliwa na UKIMWI wamepungua sana.

Aidha alifahamisha kuwa bado homa ya ini pamoja na maradhi ya Kifua kikuu  yanasumbua sana wazanzibari  na yanagharama kubwa kuyatibu, hivyo amewataka washirika maendelea mbali mbali ikiwemo USAID kuendeleza misaada yao kwa wananchi wa Zanzibar pamoja na vifaa tiba na mafunzo kwa wafanyakazi wake.

 Kwa upande wake Mshauri Mkuu wa Shirika la Misaada la  USAID Magret Toylor amesema Shirika lake litaendeleza Misaada yake kwa Zanzibar ili kuweza kuimarisha huduma za afya.

Amesema lengo  lengo la kufanya  ziara hapa nchini  nikutembelea vituo vya Afya na jumuiya wanazozisaidia .

Katika hatua nyengine  Waziri Mazrui amekutana na watendaji wa  Willow International na kuahidi kufanya kazi kwa pamoja na Wizara ya Afya ili kuweza kuimarisha huduma za kijamii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.