Habari za Punde

Dk Hussein Mwinyi ashiriki Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdalla Juma Sadala (Mabodi) alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja, kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo 20-9-2022.(Picha na Ikulu)
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dkt.Abdalla Juma Sadala (Mabodi) akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, kuongoza Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja leo 20-9-2022.(Picha na Ikulu)
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika leo 20-9-2022, katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja Jijini Zanzibar na (kulia )Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakifuatilia Kikao hicho kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, kilichofanyika leo 20-9-2022, katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAJUMBE wa Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakifuatilia Kikao hicho kikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, kilichofanyika leo 20-9-2022, katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,leo ameongoza kikao Maalum cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

 

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar.

 

Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Mapendekezo ya Wana CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Wenyeviti wa CCM Wilaya kwa Mikoa ya Zanzibar.

 

Aidha Kikao hicho Maalum, kimepokea na kujadili kwa kina Taarifa ya kazi za Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya kwa kipindi cha miaka mitano 2017/2022.

 

Pamoja na hayo Viongozi mbali mbali walioudhuria kikao hicho ni pamoja Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi,Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

 

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeil Ali Maulid pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.