Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akipokea zawadi kutoka Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke
Williams baada ya kumaliza mazungumzo
yao rasmi huko ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22.
Balozi Luke alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na
mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza
wa Rais Kitengo cha Habari.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akizungumza na
Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams ofisini kwa Makamu Migombani
mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22. Balozi Luke alifika ofisi kwa Makamu kwa
mazungumzo rasmi kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha
na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akizungumza na
Balozi wa Australia nchini Tanzania Luke Williams ofisini kwa Makamu Migombani
mjini Zanzibar leo tarehe 20.09.22. kushoto ni Helen Williams ambaye ni Balozi
Luke. Balozi huyo alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na
mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza
wa Rais Kitengo cha Habari.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Australia nchini Tanzania Luke Williams ofisini kwa Makamu Migombani mjini
Zanzibar leo tarehe 20.09.22 baada ya kumaliza mazungumzo yao rasmi. Kushoto
kwa Mhe. Makamu ni Helen Williams ambaye ni Balozi Luke. Balozi huyo alifika
ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo
mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akifurahia jambo
na Balozi wa Australia nchini Tanzania
Luke Williams baada ya kumaliza
mazungumzo yao rasmi huko ofisini kwa Makamu Migombani mjini Zanzibar leo
tarehe 20.09.22. Balozi Luke alifika ofisi kwa Makamu kwa mazungumzo rasmi
kuhusiana na mashirikiano kwenye maeneo mbali mbali . ( Picha na Ofisi ya
Makamu wa kwanza wa Rais Kitengo cha Habari
.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, asemesema kuwepo na kuendelezwa mashirikiano mazuri baina ya Serikali ya Australia na Zanzibar ni muhimu katika kuzitumia ipasavyo fursa za kiuchumi na kuendeleza utalamu wa fani mbali mbali.
Mhe. Othman
ameyasema hayo ofisini kwake Migombani mjini Zanzibar, alipokutana na Balozi wa
Austalia nchini Tanzania Luke Williams, aliyefika kwa ajili ya mazungumzo
kuhusiana na masuala mbali mbali ya mashirikiano baaina ya nchi hizo mbili.
Mhe. amesema,
Austarlia ni nchi iliyopiga hatua katika masuala mbali mbali yakiwemo ya
utaalamu kwenye fani tofauti ikiwemo sheria na taaluma nyenginezo na kwamba
Zanzibar inaweza kujifunza na kufanika sana na ushirikano kutoka nchi hiyo.
Aidha Mhe.
Makamu amesema Zanzibar imekabiliwa na changamoto kubwa za mabadiliko ya Taibia
nchi ambapo hivi sasa sehemu kadhaa za visiwa vya Zanzibar tayari zimeathirika
kwa maji kuathiri ardhi zikiwemo za kilimo na makaazi ya watu jambo ambalo
linahitaji msaada wa kiufundi ili
kujijengea uwezo katika kupamba na tatizo hilo.
Mhe. Makamu
amesema kwamba pia kuna haja ya nchi hizo kuangalia uwezekano wa kushirikiana
katika kukabiliana na tatizo la kudhibiti ukataji miti holela kwa kuwa ni suala
linaloathiri sana mazingira ikiwa ni pamoja na kuwepo mashirikiano katika
kutunza mazingira ya bahahari ili yasiendelea kuharibika.
Aidha
amesema pia aneo jengine la kuangalia mashirikiano ni pamoja na na kuwaendelea wafugaji nyuki wadogo wa
Zanzibar hasa kwa vile nchi ya Austalia inauwezo mkubwa wa kitaalamu na uzoefu
katika uzalishaji wa asali kupitia ufugaji nyuki.
Amesema
kwamba kufanya hivyo itakuwa ni fursa muhimu ya kuwasaidia wazanzibari iwapo
nchi hiyo itaamua kuwasaidia na
kuwaendelea wafugaji wadogo wa nyuki waliopo Zanzibar ikiwa ni jitihada za
kuwawezesha kuzalisha asali bora kwa wingi kwa njia ya kisasa inayoweza kukuza
soko la Zanzibar la bidhaa hiyo.
Naye Balozi
wa Australia nchini Tanzania Luke Williams, pamoja na mambo mengine ameshukuru
mashirikiano makubwa yaliyopo baina ya nchi yake na Tanzania na hasa Zanzibar
na kuahidi kwamba nchi yake ipo tayari
kuendeleza ushirikiano katika maeneo mbali mbali zikiwemo kukabiliana changamoto
za athari za mabadiliko ya tabianchi.
Amesema kwamba watanzania wengi wamepata fursa za kimasomo kwa fani mbali mbali za elimu ya juu jambo mbalo linadhihirisha na kuendelea mashirikiano ya kitaaluma na mambo mengine mbali mbali ya kimaendeleo.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari leo tarehe 20.09.02.
No comments:
Post a Comment