Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mhe.Ruto Awasili Nchini Tanzania kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Mbili

 

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege alipowasili katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akishuka kutoka katika ndege akipokea shada la Maua kutoka kwa Mtoto Tracy-Chantelle Mmbando alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto na Mke wake Mama Rachel Ruto wakizungumza na watoto Joseph Mmbando  na Tracy-Chantelle Mmbando baada ya kupokea maua  walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini


Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akisalimiana na mmoja wa maafisa waliofika ukatika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kumpokea alipowasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax wakielekea katika chumba cha mapumziko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto (kulia) Mama Rachel Ruto (wa pili kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Mhe. Alfred Mutua (wa kwanza kushoto) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchin.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Samoei Ruto amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya Siku mbili. Mhe. Dkt. Ruto ambaye ameambatana na mke wake Mama Rachel Ruto, amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, wa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam Mhe. Dkt. Ruto alikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na kuelekea hotelini kwa mapumziko.

Tarehe 10 Oktoba 2022 asubuhi, Mhe. Dkt. Ruto atawasili katika Ikulu ya Dar es salam ambapo atpokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao watakuwa na mazungumzo rasmi ambayo yatakayohusisha wajumbe wa pande zote mbili.

Baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo rasmi viongozi hao watazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na walichojadili katika ziara hiyo na baadaye watahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuandalia mgeni wake Mhe. Dkt. Ruto.

baada ya kumalizika kwa Dhifa hiyo ya Kitaifa, Mhe. Dkt. Ruto na ujumbe wake wanatarajiwa kuondoka kurejea nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.