Mlinda wa timu ya Wizara ya Elimu akijaribu kuokoa mpira ulioelekezwa langoni kwake wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Shimiwi ambapo nWizara ya Elimu iliibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Usagara
Na Oscar Assenga,TANGA.
TIMU ya Wizara ya Elimu ya Mpira wa Miguu imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Shimiwi baada ya kuifunga timu ya Wizara ya Sheria na katiba bao 1-0 katika mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika uwanja wa Usagara Jijini Tanga.
Katika mchezo huo ambao ni wa hatua ya 16 bora ,ulikuwa na ushindi mkubwa iliwalazimu timu ya Wizara ya Elimu kutumia ufundi na maarifa makubwa kuweza kuhakikisha wanaibuka na kidedea kwenye mtanange huo.
Wakicheza kwa pasi fupi fupi na ndefu Wizara ya Elimu waliweza kulitawala lango la wapinzani wao kwa dakika kadhaa na hivyo kuweza kuandika bao lao kupitia Zawadi Sanga ambaye alimaliza pasi nzuri iliyopigwa na Masoud Simba.
Baada ya kuingia kwa bao hilo timu ya Wizara ya Sheria na Katiba walirudi kujipanga ambapo walianza kuliandama lango la wapinzani wao lakini kutokana na uimara wa mabeki wake waliweza kukwama kupenya kwenye lango la Wizara ya Elimu.
Kikosi cha timu ya Wizara ya Elimu ambacho kilikuwa kikiongozwa na wachezaji mahiri kama vile Wilfred Happymaki,Yesaya Daison na Pwere Jackson waliweza kuonyesha umahiri mkubwa wa kusakata kabumbu.
Katika hatua nyengine timu ya Mchezo wa Pete ya Wizara ya Elimu imeigaragaza timu ya Wizara ya Madini kwa kuwafunga mabao 29-16.
No comments:
Post a Comment